إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ ١٠
Innal-ladhīna fatanul-mu'minīna wal-mu'mināti thumma lam yatūbū falahum 'adhābu jahannama walahum 'adhābul-harīq
Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. 10
Maelezo ya chini
10 Hakika walio watia matatani Waumini wanaume na Waumini wanawake kwa maudhi na kuwaadhibu kwa moto, kisha wasitubu na kurejea nyuma watapata Akhera adhabu ya Jahannamu kwa ukafiri wao, na watapata adhabu ya kuunguzwa kwa kule kuwaunguza moto Waumini.