Dua ya uongofu na moyo imara

Dua za uongofu, uchamungu na moyo unaobaki imara katika imani.

1 Mara moja

اللَّهُمَّ اهْدِنِي وَسَدِّدْنِي

Maana na chanzo

Kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuamrisha Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake amtake Mwenyezi Mungu na amuombe na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu niongoze" na unielekeze na unijulishe "na unisimamie" na uniafikishe, na unifanye kuwa na msimamo katika mambo yangu yote.

Uongofu: Ni kuijua haki kwa ujumla na kwa ufafanuzi, na kuwezeshwa kuifuata kwa wazi na kwa siri.

Na kusimamiwa: Ni kuwezeshwa na kuwa na msimamo katika mambo yote katika yale ya kweli juu ya haki, nayo ni njia iliyonyooka katika kauli na vitendo na itikadi.

Na hii ni kwa sababu jambo lisiloonekana hueleweka wazi kupitia jambo linaloonekana; Hivyo kumbuka unapokuwa unaomba dua hii kuwa: "Uongofu: Ni kuongozwa njia" Hivyo, hudhurisha moyo wako nawe ukiwa unaomba uongofu mfano wa uongofu wa aliyesafarini, kwani huwa hatoki nje ya njia si kulia wala kushoto; na hii ni ili asalimike na kupotea, na kwa hilo anapata usalama, na atafika haraka katika lengo lake.

"Na kuafikishwa nakupatia: Ni kupatia kwa mshale" Wewe chunguza wakati wa kulenga kwako mshale katika uharaka wa kufika kwake na kukipata ulichokusudia kukipiga, mrusha mishale anaporusha katika lengo basi huhakikisha ameulenga vizuri mshale katika kile alichokikusudia, hivyo hivyo na wewe unamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa yote unayoyakusudia basi yawe katika mfano wa mshale; utakuwa katika kuomba kwako umeomba kiwango cha juu zaidi cha uongofu, na mwisho wa kusimamiwa.

Vuta picha ya maana hii kwa moyo wako ili umuombe usimamizi Mwenyezi Mungu na kupatia katika mambo yako, ili yale unayoyanuia katika hilo yawe katika mfano wa namna unavyofanya mshale.

Faida

  • Muombaji anatakiwa apupie kupatia katika amali yake na kuinyoosha kwa kushikamana na sunna na kutakasa nia.
  • Sunna ya kuomba dua kwa maneno haya yaliyokusanya kuwezeshwa na kusimamiwa katika mambo.
  • Ni wajibu kwa mja kutaka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yake yote.
  • Kupiga mifano wakati wa kufundisha.
  • Kukusanya kati ya kutaka uongofu na kutengenezewa na hali, na kudumu juu yake na kutopotoka hata chembe ndogo na kutengemaa kwa mafikio, hivyo kauli yake: "Niongoze" Ili nitembee juu ya njia ya uongofu, na kauli yake: "Na unisimamie" ni katika kupatia na kutopotoka wakati wa uongofu uliomfika.
  • Muombaji anatakiwa aitilie maanani dua yake, na avute picha ya maana ya maombi yake ndani ya moyo wake; kwani hili huleta msukumo mkubwa wa kujibiwa dua.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْهُدَى وَالتُّقَى، وَالْعَفَافَ وَالْغِنَى

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.

Faida

  • Utukufu wa mambo haya: Uongofu, uchamungu, na kujizuia na machafu, na kutosheka, na himizo la kujipamba nayo.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake hamiliki juu ya nafsi yake manufaa wala madhara, na kwamba anayemiliki hayo ni Allah Mtukufu.
  • Anayemiliki manufaa na madhara na uongofu kwa viumbe ni Mwenyezi Mungu peke yake, si Malaika aliyekaribu wala Mtume aliyetumwa wala yeyote asiyekuwa wao.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

اللهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي الَّتِي فِيهَا مَعَادِي، وَاجْعَلِ الْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْرٍ، وَاجْعَلِ الْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa dua iliyokusanya ndani yake misingi ya tabia njema alizotumwa kuzitimiliza; nazo ni kutengenezewa dini, na dunia, na Akhera, akachota kutoka katika matamshi haya mafupi kutengemaa kwa mambo makubwa matatu, na akaanza na kutengemaa kwa dini, ambayo ndiyo sababu ya kutengemaa hali ya Dunia na Akhera, akasema:

"Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu" Kwa kuniafikisha kusimamia adabu zake kwa namna iliyokamilika na kutimia zaidi.

"Ambayo ndiyo ngome ya jambo langu" Na iwe hifadhi kwa mambo yangu yote, ikiwa dini yangu itaharibika basi yataharibika mambo yangu, na nitapata hasara na kutoka patupu, na kwakuwa hakuwezi kutimia kutengemaa kwa dini inayotakiwa isipokuwa kwa kutengemaa dunia, akasema:

"Na unitengenezee dunia yangu" Kwa kunipa afya ya mwili na amani, na riziki, na mke mwema, na kizazi kizuri na yale ninayoyahitaji, na yawe ya halali, na yanisaidie katika kukutii, kisha akataja udhuru katika kuomba kwake kutengemaa kwake; kwa kusema:

"Ambayo kuna maisha yangu" Na mahala pa kuishi kwangu na muda wa uhai wangu.

"Na unitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu" Na kurejea kwangu ili kukutana na wewe, na hii ni kwa kutengemaa kwa matendo, na Mwenyezi Mungu kumuwezesha mja katika ibada na ikhlasi, na kuupata mwisho mwema.

Na akapangilia rehema na amani ziwe juu yake Akhera baada ya dunia; kwa sababu ya kwanza ndio sababu ya kutengemaa ya pili, atakayekuwa na msimamo katika dini yake kwa namna atakavyo Mwenyezi Mungu, basi Akhera yake itanyooka na atapata furaha ndani yake.

"Na uufanye uhai" Yaani: Na kurefushwa kwa umri "Kuwa ni ziada kwangu katika kila kheri" Ili nizidishe amali njema, "Na uyafanye mauti" na kuharakishwa kwake "Raha kwangu kutokana na kila shari" Na fitina na mitihani na majaribu kwa maasi na kughafilika, na ili iwe ni sababu ya kuepukana na matatizo ya Dunia na shida zake, na kupatikana kwa raha.

Faida

  • Dini ndio kitu muhimu; na ndio maana alianza nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua.
  • Dini ndio ngao ya mwanadam inayomkinga dhidi ya kila shari.
  • Kuomba mambo ya kidunia kwa ajili ya kutengeneza dini na Akhera.
  • Si vibaya kutamani kufa kwa kuhofia mitihani na fitina katika dini, au kumuomba Mwenyezi Mungu kufa katika shahada.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"

Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upotofu. Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake alistaajabu kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiiomba dua hii mara kwa mara, basi Mtume rehema na amani zimshukie akamwambia kuwa nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, huzigeuza apendavyo, hivyo, moyo ni kituo cha imani na ukafiri, na moyo umeitwa Qalbu kwa sababu ya kugeukageuka kwake mara kwa mara, moyo hugeuka sana kuliko chungu kinapokusanyika kile kinachotokota ndani yake. Amtakaye Mwenyezi Mungu huudumisha moyo wake katika uongofu na uthabiti katika Dini, na anayemtaka Mwenyezi Mungu huugeuza moyo wake kutoka katika uongofu na kuupeleka katika upotofu.

Faida

  • Kujisalimisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na kunyenyekea kwake, na kuuelekeza umma kuliomba hilo.
  • Umuhimu wa kuwa na msimamo na uthabiti katika dini, na kuwa kinachozingatiwa ni hatima ya mtu ya maisha yake.
  • Mja hawezi kujitosheleza mwenyewe hata kwa kupepesa jicho bila ya kutiwa uthabiti na Mwenyezi Mungu katika Uislamu.
  • Himizo la kuomba dua hii kwa wingi, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Kudumu katika Uislamu ni neema kubwa ambayo mja anatakiwa kuifanyia juhudi na kumshukuru Mola wake Mlezi.

Soma kwenye HadeethEnc.com

5 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amri bin Aaswi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako" Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika kukutii".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili katika vidole vya Rahmaan kama moyo mmoja; anaugeuza kokote atakako; akitaka anausimamisha katika haki, na akitaka anaupotoa katika haki, na kuzigeuza kwake nyoyo zote ni kama kuugeuza moyo mmoja, hakuna jambo linaloweza kumshughulisha akaacha jambo jingine, kisha akaomba rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, wakati mwingine katika utiifu na wakati mwingine katika maasi, na wakati mwingine katika kukutaja na wakati mwingine katika kughafilika, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika utiifu wako.

Faida

  • Kumethibitishwa makadirio, nakuwa Mwenyezi Mungu anazielekeza nyoyo za waja wake kulingana na kadari aliyoziandikia juu yake.
  • Inampasa muislamu kudumu kumuomba Mola wake Mlezi kuthubutu katika haki na uongofu.
  • Kumhofu Mwenyezi Mungu na kufungamana nayeye peke yake asiye na mshirika.
  • Amesema Aajurri: Hakika watu wa haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa alizojisifu mwenyewe Aliyetakasika na kutukuka, na kwa sifa alizomsifu kwazo Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa zile walizomsifu kwazo Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale waliofuata muongozo na wala hawakuzua. Mwisho. Watu wa sunna humthibitishia Mwenyezi Mungu aliyoyathibitisha yeye mwenyewe kwa nafsi yake katika majina na sifa pasina kupotoa, wala kukanusha wala kuhoji wala kufananisha, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha yeye mwenyewe juu nafsi yake, na wananyamaza katika yale ambayo mafundisho hayakueleza kuthibitisha au kukanusha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna chochote mfano wake, naye ni Msikivu Mwenye kuona".

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya uongofu: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.