Surat Al-'Adiyat العاديات

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا ١

Wal-'ādiyāti dabhā

Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, 1

فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا ٢

Fal-mūriyāti qadhā

Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, 2

فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا ٣

Fal-mughīrāti subhā

Wakishambulia wakati wa asubuhi, 3

فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا ٤

Fa atharna bihī naq'ā

Huku wakitimua vumbi, 4

فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا ٥

Fawasatna bihī jam'ā

Na wakijitoma kati ya kundi, 5

إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٞ ٦

Innal-insāna lirabbihī lakanūd

Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! 6

وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٞ ٧

Wa innahū 'alā dhālika lashahīd

Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! 7

وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلۡخَيۡرِ لَشَدِيدٌ ٨

Wa innahū lihubbil-khayri lashadīd

Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! 8

۞ أَفَلَا يَعۡلَمُ إِذَا بُعۡثِرَ مَا فِي ٱلۡقُبُورِ ٩

Afalā ya'lamu idhā bu'thira mā fil-qubūr

Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? 9

وَحُصِّلَ مَا فِي ٱلصُّدُورِ ١٠

Wahussila mā fis-sudūr

Na yakakusanywa yaliomo vifuani? 10

إِنَّ رَبَّهُم بِهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّخَبِيرُۢ ١١

Inna rabbahum bihim yawma'idhil lakhabīr

Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! 11

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-'Adiyat ina aya ngapi?

Surat Al-'Adiyat ina aya 11. Ni sura namba 100 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-'Adiyat ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-'Adiyat ni sura Makkiya.

Surat Al-'Adiyat iko katika juzuu gani?

Surat Al-'Adiyat iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-'Adiyat?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.