Surat Nuh نوح

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرۡ قَوۡمَكَ مِن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ١

Innā arsalnā nūhan ilā qawmihī an andhir qawmaka min qabli an ya'tiyahum 'adhābun alīm

Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu. 1

قَالَ يَٰقَوۡمِ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ ٢

Qāla yāqawmi innī lakum nadhīrum mubīn

Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu! 2

أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ ٣

Ani'budullāha wattaqūhu wa atī'ūn

Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii. 3

يَغۡفِرۡ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُؤَخِّرۡكُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُۚ لَوۡ كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ٤

Yaghfir lakum min dhunūbikum wayu'akkhirkum ilā ajalim musamman inna ajalallāhi idhā jā'a lā yu'akkharu law kuntum ta'lamūn

Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua! 4

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوۡتُ قَوۡمِي لَيۡلٗا وَنَهَارٗا ٥

Qāla rabbi innī da'awtu qawmī laylan wanahārā

Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana! 5

فَلَمۡ يَزِدۡهُمۡ دُعَآءِيٓ إِلَّا فِرَارٗا ٦

Falam yazidhum du'ā'ī illā firārā

Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia. 6

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوۡتُهُمۡ لِتَغۡفِرَ لَهُمۡ جَعَلُوٓاْ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَٱسۡتَغۡشَوۡاْ ثِيَابَهُمۡ وَأَصَرُّواْ وَٱسۡتَكۡبَرُواْ ٱسۡتِكۡبَارٗا ٧

Wa innī kullamā da'awtuhum litaghfira lahum ja'alū asābi'ahum fī ādhānihim wastaghshaw thiyābahum wa asarrū wastakbarustikbārā

Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno! 7

ثُمَّ إِنِّي دَعَوۡتُهُمۡ جِهَارٗا ٨

Thumma innī da'awtuhum jihārā

Tena niliwaita kwa uwazi! 8

ثُمَّ إِنِّيٓ أَعۡلَنتُ لَهُمۡ وَأَسۡرَرۡتُ لَهُمۡ إِسۡرَارٗا ٩

Thumma innī a'lantu lahum wa asrartu lahum isrārā

Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri. 9

فَقُلۡتُ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارٗا ١٠

Faqultustaghfirū rabbakum innahū kāna ghaffārā

Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. 10

يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا ١١

Yursilis-samā'a 'alaykum midrārā

Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. 11

وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّٰتٖ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡهَٰرٗا ١٢

Wayumdidkum bi amwālin wabanīna wayaj'al lakum jannātin wayaj'al lakum anhārā

Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito. 12

مَّا لَكُمۡ لَا تَرۡجُونَ لِلَّهِ وَقَارٗا ١٣

Mmā lakum lā tarjūna lillāhi waqārā

Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu? 13

وَقَدۡ خَلَقَكُمۡ أَطۡوَارًا ١٤

Waqad khalaqakum atwārā

Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja? 14

أَلَمۡ تَرَوۡاْ كَيۡفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ طِبَاقٗا ١٥

Alam taraw kayfa khalaqallāhu sab'a samāwātin tibāqā

Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka? 15

وَجَعَلَ ٱلۡقَمَرَ فِيهِنَّ نُورٗا وَجَعَلَ ٱلشَّمۡسَ سِرَاجٗا ١٦

Waja'alal-qamara fīhinna nūran waja'alash-shamsa sirājā

Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa? 16

وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ نَبَاتٗا ١٧

Wallāhu ambatakum minal-ardi nabātā

Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea. 17

ثُمَّ يُعِيدُكُمۡ فِيهَا وَيُخۡرِجُكُمۡ إِخۡرَاجٗا ١٨

Thumma yu'īdukum fīhā wayukhrijukum ikhrājā

Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena. 18

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ بِسَاطٗا ١٩

Wallāhu ja'ala lakumul-arda bisātā

Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati. 19

لِّتَسۡلُكُواْ مِنۡهَا سُبُلٗا فِجَاجٗا ٢٠

Llitaslukū minhā subulan fijājā

Ili mtembee humo katika njia zilizo pana. 20

قَالَ نُوحٞ رَّبِّ إِنَّهُمۡ عَصَوۡنِي وَٱتَّبَعُواْ مَن لَّمۡ يَزِدۡهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارٗا ٢١

Qāla nūhur rabbi innahum 'asawnī wattaba'ū mal lam yazidhu māluhū wawaladuhū illā khasārā

Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara. 21

وَمَكَرُواْ مَكۡرٗا كُبَّارٗا ٢٢

Wamakarū makran kubbārā

Na wakapanga vitimbi vikubwa. 22

وَقَالُواْ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمۡ وَلَا تَذَرُنَّ وَدّٗا وَلَا سُوَاعٗا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسۡرٗا ٢٣

Waqālū lā tadharunna ālihatakum walā tadharunna waddan walā suwā'an walā yaghūtha waya'ūqa wanasrā

Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra. 23

وَقَدۡ أَضَلُّواْ كَثِيرٗاۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَٰلٗا ٢٤

Waqad adallū kathīran walā tazidiz-zālimīna illā dalālā

Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea. 24

مِّمَّا خَطِيٓـَٰٔتِهِمۡ أُغۡرِقُواْ فَأُدۡخِلُواْ نَارٗا فَلَمۡ يَجِدُواْ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارٗا ٢٥

Mmimmā khatī'atihim ughriqū fa udkhilū nāran falam yajidū lahum min dūnillāhi ansārā

Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu. 25

وَقَالَ نُوحٞ رَّبِّ لَا تَذَرۡ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ دَيَّارًا ٢٦

Waqāla nūhur rabbi lā tadhar 'alal-ardi minal-kāfirīna dayyārā

Na Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri! 26

إِنَّكَ إِن تَذَرۡهُمۡ يُضِلُّواْ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓاْ إِلَّا فَاجِرٗا كَفَّارٗا ٢٧

Innaka in tadharhum yudillū 'ibādaka walā yalidū illā fājiran kaffārā

Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri. 27

رَّبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيۡتِيَ مُؤۡمِنٗا وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارَۢا ٢٨

Rrabbighfir lī waliwālidayya waliman dakhala baytiya mu'minan walil-mu'minīna wal-mu'mināti walā tazidiz-zālimīna illā tabārā

Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea. 28

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Aya maarufu

Maswali

Surat Nuh ina aya ngapi?

Surat Nuh ina aya 28. Ni sura namba 71 ya Qur'ani.

Je, Surat Nuh ni Makkiya au Madaniya?

Surat Nuh ni sura Makkiya.

Surat Nuh iko katika juzuu gani?

Surat Nuh iko katika juzuu 29.

Je, naweza kusikiliza Surat Nuh?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.