Istaghfiru rabbakum

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

فَقُلۡتُ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارٗا ١٠

Faqultustaghfirū rabbakum innahū kāna ghaffārā

Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. 10

Maelezo ya chini

10 Nikawambia watu wangu: Takeni kwa Mola wenu Mlezi maghfira kwa kufru zenu na maasi yenu. Kwani Yeye bado ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya mwenye kurejea kwake.

يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا ١١

Yursilis-samā'a 'alaykum midrārā

Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. 11

Maelezo ya chini

11 Atakuleteeni mawingu yatakayo miminika mvua kwa wingi,

وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّٰتٖ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡهَٰرٗا ١٢

Wayumdidkum bi amwālin wabanīna wayaj'al lakum jannātin wayaj'al lakum anhārā

Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito. 12

Maelezo ya chini

12 Na atakupeni mali na wana, na hayo ndiyo mapambo ya dunia, na atakupeni mashamba mtayo starehea kwa uzuri wake na matunda yake, na atakujaalieni mito ya kunyweshea mazao yenu na mifugo yenu.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Nuh yote

Maswali

Istaghfiru rabbakum iko wapi katika Qur'ani?

Istaghfiru rabbakum iko katika Surat Nuh, 71:10-12.