Swalawat: kumswalia Mtume ﷺ

Jinsi ya kumswalia Mtume ﷺ, na malipo yake.

1 Mara moja

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ، اللَّهُمَّ بَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Masahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu namna ya kumtakia rehema? baada ya kujua kwao namna kumuombea amani (salam) katika kikao cha tahiyatu ndani ya swala: "Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake...?" Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akawaeleza namna ya kumtakia rehema, na maana yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad na juu ya watu wa Muhammad" Yaani: Mtaje kwa sifa nzuri kwa Malaika walioko juu mbinguni, na juu ya wafuasi wake katika dini yake, na waumini katika ndugu zake wa karibu. "Kama ulivyoteremsha rehema juu ya watu wa Ibrahim" Kama ulivyotoa takrima juu ya watu wa Ibrahim amani iwe juu yake, nao ni Ibrahim na Ismail na Is'haka na kizazi chake na wafuasi wao miongoni mwa waumini, basi zipeleke fadhila zako kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake. "Hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa". Yaani: Mwenye kuhimidiwa katika dhati yako na sifa zako na vitendo vyako, mpana katika utukufu wako na ugawaji riziki wako. "Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na juu ya watu wa Muhammad kama ulivyoteremsha baraka juu ya watu wa Ibrahim" Yaani: Mpe katika kheri na karama zile zilizo kubwa zaidi na uzizidishe na umdumishie kheri hizo.

Faida

  • Wema waliotangulia walikuwa wakizawadiana kuhusu mambo ya elimu.
  • Uwajibu wa kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika tashahudi ya mwisho katika swala.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwafundisha Masahaba wake kumtakia amani na rehema juu yake.
  • Namna hii ya kuomba ndio namna sahihi zaidi katika kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Hussein bin Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia"

Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kumtakia rehema wakati wa kusikia jina lake au wasifu wake, na akasema: Bahili kamili ni yule nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema; na hili ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:

La kwanza: Nikuwa ni ubahili kwa kitu ambacho mtu hapati hasara sawa iwe ndogo au kubwa, wala hatoi mali, na wala hatumii nguvu wala juhudi.

La pili: Ni kuifanyia ubahili nafsi yake kwa sababu anainyima malipo ya kumtakia rehema Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake: kwa sababu anapojizuia kumtakia rehema atakuwa kafanya ubahili na kakataa kutimiza haki ya wajibu kwake kuitekeleza, kwa kutekeleza amri na akapata malipo.

La tatu: Kumtakia rehema ndani yake kuna kutimiza haki za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yeye ndiye aliyetufundisha, na yeye ndiye aliyetuelekeza, na yeye ndiye aliyetuita kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaja na wahyi huu, na sheria hii, yeye ndiye sababu ya kuongoka kwetu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, atakayeacha kumtakia rehema basi atakuwa kamfanyia ubahili Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutompa haki ndogo kabisa miongoni mwa haki zake

Faida

  • Kuacha kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni miongoni mwa alama za ubahili.
  • Kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni katika ibada bora anazojikurubisha kwazo mja katika nyakati zote, na inatiwa mkazo hasa wakati wa kutajwa kwake.
  • Amesema Imam Nwawi: Mtu akimsalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi akusanye kati ya kumsalia na kumtakia amani, na wala asiishie katika moja ya haya; Asiseme: "Rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake" Pekee, wala: "Amani iwe juu uake" pekee.
  • Amesema Abul Aalia katika kauli yake: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii" Akasema: Sala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake: Ni kumsifia, na sala ya Malaika na watu: Ni kumuombea dua.
  • Amesema Al-Hulaimi: Maana ya "Ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammad": Ewe Mwenyezi Mungu mtukuze katika dunia kwa kukuza kutajwa kwake, na kuidhihirisha dini yake, na kuibakiza sheria yake, na Akhera: Kwa kumfanya kuwa mtetezi wa umma wake, na kuyajaza malipo yake na thawabu zake, na kwa kuzionyesha wazi fadhila zake kwa wa mwanzo na wa mwisho kwa kumpa nafasi nzuri, na kwa kumtanguliza mbele kuliko wote waliokaribu nawe watakaoshuhudia Kiyama.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi".

Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Makundi matatu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyaombea dua mbaya ya pua zao kugusa mchanga kwa udhalili na unyonge na hasara: Kundi la kwanza: Yule atakayetajwa mbele yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akawa hakumswalia, kwa kusema: Swalla llaahu a'laihi wasallam (Rehema na amani ziwe juu yake) na mfano wake. La pili: Ni yule atakayeupata mwezi wa Ramadhani kisha mwezi ukamalizika kabla hajasamehewa kwa uzembe wake wa kufanya mambo ya kheri. La tatu: Ni mtu atakayewapata wazazi wake wakiwa watu wazima, na hawakuwa sababu ya yeye kuingia peponi kwa sababu ya kuwaasi kwake na uzembe wake katika kutekeleza haki zao.

Faida

  • Amesema As-Sanadi: Kiuhalisia nikuwa kila mmoja katika hawa kapata jambo ambalo lau kama si uzembe basi angepata fungu kubwa katika kheri, wakati alipofanya uzembe mpaka likampita hilo basi atakuwa amefeli na kupata hasara.
  • Himizo la kumswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kila linapotajwa jina lake.
  • Himizo la kujitahidi na kujikaza katika ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani.
  • Himizo la kufanya juhudi kubwa katika kuwatendea wema wazazi wawili na kuwakirimu, hasa hasa wakati wa uzee.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Swalawat kwa Mtume ﷺ: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.