Dua ya wasiwasi, hofu na dhiki

Dua alizoomba Mtume ﷺ katika shida na alizofundisha kwa wasiwasi na huzuni.

1 Mara moja

لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ الْعَظِيمُ الْحَلِيمُ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَرَبُّ الْأَرْضِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema wakati wa matatizo: "Laa ilaaha illa llaahul a'dhwiimul haliim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbul A'rshil A'dhwiim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbu ssamaawaati warabbul A'rshil kariim" Tafsiri: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mpole, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa A'rshi tukufu, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa A'rshi takatifu".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema wakati wa kuzidi kwa matatizo na huzuni kwake: "Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" Hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Mtukufu" wa cheo, Mtukufu wa shani, katika dhati yake na sifa zake na majina yake, "Mpole" asiyemharakisha mwenye kuasi kwa kumpa adhabu bali anaichelewesha, na anaweza kumsamehe pamoja nakuwa anauwezo wa kumuadhibu, yeye ndiye muweza Mtukufu juu ya kila kitu ni muweza. "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa Arshi tukufu" Muumba wa Arshi tukufu, "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa mbingu na ardhi" na muumba wa mbingu na ardhi, na muumba wa kila kitu ndani yake na mmiliki wake na mrekebishaji wake, na mwenye maamuzi ndani yake kwa namna yoyote aitakayo, "Mola wa Arshi karim" Muumba wa Arshi karim.

Faida

  • Uwajibu wa kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu kwa dua wakati wa kufikwa na misiba na matatizo.
  • Kupendeza kuomba dua hii wakati wa matatizo.
  • Arshi ya Rahmaan (Mwingi wa rehema) aliyotulizana juu yake Aliyetakasika na kutukuka, ndio kiumbe cha juu zaidi kuliko vyote, na kikubwa zaidi na kitukufu zaidi kuliko vyote, na alitoa wasifu wake Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni kubwa na ni tukufu.
  • Zimetajwa mbingu na ardhi pekee; kwa sababu ni katika viumbe vikubwa zaidi katika vile vinavyoonekana.
  • Amesema Attwayyibi: Ametanguliza sifa hii kwa kumtaja Mola Mlezi ili iendane na kutatua shida; kwa sababu ndilo neno linaloendana na malezi, na ndani yake kuna tahlil (kauli ya Laa ilaaha illa llaah) iliyokusanya tauhidi ambayo ndiyo asili ya kutakasa utukufu wake, na utukufu ambao unaonyesha utimilifu wa uwezo, na upole ambao unaonyesha kuwa na elimu, kwa sababu mjinga hatuwezi kuvuta picha kuwa anaweza kuwa na upole wala ukarimu kwa vitu asivyovijua, nazo ndio asili ya sifa na ukarimu.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ، وَشَمَاتَةِ الْأَعْدَاءِ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"

Imepokelewa na Nasai na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na mambo haya:

La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda" na ninajikabidhi na kujiweka "kwako" si kwa mwingine, "kutokana na kuelemewa na deni" na kunitenza nguvu na misukosuko yake, na ninakuomba msaada wa kulilipa na kulitimiza.

La pili: "Na kuzidiwa na adui" na kunitenza nguvu na kunitawala kimabavu, na ninakuomba uzuie adha zake, na unipe ushindi juu yake.

La tatu: "Na kutukanwa na maadui" na kufurahi kwao kwa yale yanayowafika waislamu miongoni mwa mabalaa na misiba.

Faida

  • Himizo la kutaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na yote yanayomshughulisha mtu na ibada na kuleta msongo wa mawazo kama madeni na mengineyo.
  • Deni la kawaida halina tatizo, isipokuwa tatizo ni kwa yule asiyekuwa na mali ya kulipa deni, na hili ndio deni linaloelemea.
  • Mwanadam anatakiwa ayaepuke mambo yanayopelekea kutukanwa au kuabishwa kwayo.
  • Kumebainishwa uadui wa makafiri kwa waumini na kufurahishwa kwao pale wanapofikwa na majanga.
  • Maadui kudhihirisha furaha yao kwa mtihani wa mtu hili humuongezea maumivu makubwa kuliko hata balaa lenyewe.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya wasiwasi na dhiki: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.