Dua ya kulipa deni

Dua za kuondokewa na deni na kupata riziki ya halali.

1 Mara moja

اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba mtu mmoja aliyeandikishana kujitoa katika utumwa alimjia akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni tuliloandikishana, basi naomba unisaidie, akasema: Je, nikufundishe maneno ambayo alinifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hata kungekuwa juu yako na deni zito mfano wa mlima Swiri Mwenyezi Mungu atakulipia, akasema: "Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe.

Imepokelewa Imamu Tirmidhiy Daraja: Ni nzuri (Hasan)

Maelezo

Alimuijia kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake bwana mmoja mtumwa alikuwa kaandikishana na bwana yake na amekubaliana naye ili aikomboe nafsi yake na aiache huru ili awe huru, na hakuwa na mali, akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni hilo juu yangu, nakuomba unisaidie kulilipa kwa mali, au kwa kunifundisha na kunielekeza, akasema kumwambia kiongozi wa waumini: Je, nikufundishe maneno aliyonifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lau kama ungelikuwa na deni mfano wa mlima Swiri wa kabila la Twayyi basi Mwenyezi Mungu angelikulipia kwa mstahiki wake, na angelikuokoa kutoka katika madhila yake, akasema: Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze" na uniepushe na uniweke mbali "kwa halali yako" nitosheke nayo "dhidi ya" kutumbukia katika "haramu yako", na unitosheleze "kwa fadhila zako" na ukarimu wako "kutomuhitaji yeyote" katika viumbe.

Faida

  • Kuomba ushauri na kutaka rai ya wasomi wa dini.
  • Ni juu ya wasomi na walimu wa dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa muongozo walinganiaji, na kuwaelekeza katika yale yanayoweza kuwasaidia kwa yale yanayowatokea miongoni mwa matatizo.
  • Himizo la kumsaidia mwenye mkataba.
  • Himizo la kujifunza dua hii, na kumuomba Allah kupitia dua hii.
  • Riziki ya halali hata ikiwa ndogo, ni bora kuliko mali ya haramu hata ikiwa nyingi.
  • Kutosheka na Mwenyezi Mungu na kuwaacha viumbe.
  • Himizo la kumjibu muombaji kwa majibu mazuri ikiwa huna cha kumpa.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ، وَشَمَاتَةِ الْأَعْدَاءِ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"

Imepokelewa na Nasai na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na mambo haya:

La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda" na ninajikabidhi na kujiweka "kwako" si kwa mwingine, "kutokana na kuelemewa na deni" na kunitenza nguvu na misukosuko yake, na ninakuomba msaada wa kulilipa na kulitimiza.

La pili: "Na kuzidiwa na adui" na kunitenza nguvu na kunitawala kimabavu, na ninakuomba uzuie adha zake, na unipe ushindi juu yake.

La tatu: "Na kutukanwa na maadui" na kufurahi kwao kwa yale yanayowafika waislamu miongoni mwa mabalaa na misiba.

Faida

  • Himizo la kutaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na yote yanayomshughulisha mtu na ibada na kuleta msongo wa mawazo kama madeni na mengineyo.
  • Deni la kawaida halina tatizo, isipokuwa tatizo ni kwa yule asiyekuwa na mali ya kulipa deni, na hili ndio deni linaloelemea.
  • Mwanadam anatakiwa ayaepuke mambo yanayopelekea kutukanwa au kuabishwa kwayo.
  • Kumebainishwa uadui wa makafiri kwa waumini na kufurahishwa kwao pale wanapofikwa na majanga.
  • Maadui kudhihirisha furaha yao kwa mtihani wa mtu hili humuongezea maumivu makubwa kuliko hata balaa lenyewe.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya deni: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.