Dua ya hasara na msiba (Inna lillahi)

Unachosema hasara au shida inapotokea, na maneno ya kuwafariji waliofiwa.

1 Mara moja

إِنَّا لِلهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي، وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا

Maana na chanzo

Kutoka kwa Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo" Akasema: Alipofariki Abuu Salama, nikasema: Ni Muislamu gani atakuwa bora kuliko Abuu Salama? Nyumba ya kwanza aliyohamia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi nikasema maneno hayo, Mwenyezi Mungu akanipa mbadala wake ambaye ni Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza mama wa waumini Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema siku moja: Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyopendezeshewa na Mwenyezi Mungu kwake kuyasema: "Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea" [Baqara: 156], "Ewe Mwenyezi Mungu nilipe" na unipe malipo ya subira yangu "katika msiba wangu", na unipe badala "na unirejeshee" kwa hilo "kheri kuliko hiyo"; isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa mbadala bora kuliko hilo. Akasema: Alipofariki Abuu Salama akasema: Ni nani katika Waislamu atakuwa bora kuliko Abuu Salama?! Nyumba ya kwanza iliyohama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi Mwenyezi Mungu alinisaidia nikaisema kauli hiyo, Mwenyezi Mungu akanipa badala Mtume rehema na amani ziwe juu yake bora zaidi kuliko Abuu Salama.

Faida

  • Amri ya kuwa na subira wakati wa mitihani masaibu na kutopaparika.
  • Kuelekeza dua kwa Mwenyezi Mungu katika mambo mazito; kwa sababu kwake ndio kuna mbadala.
  • Umuhimu wa waumini kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hata isipojulikana hekima yake.
  • Kheri yote kwa muumini iko katika kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya msiba: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.