Dua ya kupiga chafya na jibu lake

Anachosema anayepiga chafya, na anachojibu anayemsikia.

1 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu ni mambo sita: La kwanza: Amsalimie akikutana naye kwa kusema: Assalaam alaikum, naye atajibu salamu kwa kusema: Waalaikumussalaam. La pili: Kuitika wito wake atakapomuita kwa ajili ya sherehe ya harusi au nyingineyo. La tatu: Kumpa nasaha akizihitajia, na wala usimsifie bure, au kumfanyia udanganyifu. La nne: Akipiga chafya akasema: Alhamdulillaah, basi muombee dua kwa kusema: Yar-hamkallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu), naye ajibu kwa kusema: Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum (Akuongozeni Mwenyezi Mungu na kutengenezeeni hali zenu). La tano: Akamuone na amtembelee atakapougua. La sita: Amswalie atakapofariki, na alisindikize jeneza lake mpaka azikwe.

Faida

  • Amesema Shaukani: Na makusudio ya kauli yake: (Haki za muislamu) Nikuwa haitakiwi kuziacha, na kunakuwa kuzifanya kwake ima ni wajibu au sunna iliyotiwa mkazo inayofanana na wajibu ambayo haitakikani kuiacha.
  • Kujibu salamu ni faradhi ya lazima, mwenye kusalimiwa atakapokuwa mmoja, na wakiwa wengi basi mmoja anatosheleza, ama kuanza salamu asili yake ni sunna.
  • Mgonjwa kutembelewa ni katika haki zake juu ya ndugu zake waislamu; kwa sababu humuingizia furaha na liwazo ndani ya moyo wake, na ni faradhi ya kujitosheleza, wakifanya wenye kutosheleza basi wengine hawana dhambi.
  • Uwajibu wa kuitika wito kukiwa hakuna madhmbi ndani yake; ikiwa ni wito wa sherehe ya harusi basi jopo la wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kuitika, isipokuwa kukiwa na udhuru wa kisheria, ama ikiwa si sherehe ya harusi jopo la wanachuoni wakasema kuwa ni sunna.
  • Kumuombea dua aliyepiga chafya ni wajibu juu ya yule aliyesikia kumhimidiwa Mwenyezi Mungu mpiga chafya.
  • Ukamilifu wa sheria na pupa yake katika kuunganisha nguvu na umoja wa jamii na imani, na nyenzo za mapenzi kati ya mtu mmoja mmoja.
  • "Muombee rehema" Yaani kumuombea dua ya kheri na baraka, na tashmiiti (kumuombea dua) imesemekana maana yake: Mwenyezi Mungu akuweke mbali na kuchekwa na maadui, na ayaweke mbali nawe yale yatakayofanya adui yako akucheke, na tasmiit (kwa siin): Maana yake: Mwenyezi Mungu akuongoze katika ustaarabu ulionyooka.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya:

Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywani mwake au puani mwake chochote kitakachomuudhi aliyekaa naye.

Jambo la pili: Anashusha sauti yake na wala hainyanyui.

Faida

  • Hapa pamebainishwa muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake, ikiwa ni pamoja na kumuiga katika hilo.
  • Inapendekeza kuweka nguo au leso au mfano wa hayo mdomoni na puani mtu anapopiga chafya, ili kitu chochote kisitoke humo kitakachomuudhi mtu aliyekaa naye.
  • Kupunguza sauti ya mtu wakati wa kupiga chafya kunahitajika, na ni ishara ya adabu kamili na maadili mema.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya kupiga chafya: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.