Dua ya mgonjwa na ya kumtembelea mgonjwa

Unachosema unapomtembelea mtu aliye mgonjwa.

1 mara 7

أَسْأَلُ اللَّهَ الْعَظِيمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ أَنْ يَشْفِيَكَ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hakuna muislamu atakayemtembelea muislamu katika maradhi yake, ambaye muda wa mauti yake haujafika, kisha aliyekwenda kumtembelea akamuombea mgonjwa kwa kusema: "Namuomba Allah Mtukufu" katika dhati yake na sifa zake na vitendo vyake, "Mola wa Arshi Tukufu akuponye", na akarudia mbele yake mara saba, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kutokana na maradhi hayo.

Faida

  • Inapendeza kumuombea mgonjwa kwa dua hii, na kuirudiarudia mara saba.
  • Kupatikana kwa ponyo kwa atakayeombewa mbele yake dua hii kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikisomwa kwa dhati na kwa mtu mwema.
  • Ataisoma dua hii kwa siri na kwa wazi, yote hiyo inafaa, lakini akimsikilizisha mgonjwa ndiyo bora zaidi; kwa sababu katika hilo kuna kuingiza furaha kwake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

أَذْهِبِ الْبَاسَ، رَبَّ النَّاسِ، وَاشْفِ أَنْتَ الشَّافِي، لَا شِفَاءَ إِلَّا شِفَاؤُكَ، شِفَاءً لَا يُغَادِرُ سَقَمًا

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomtembelea mgonjwa anamuombea dua kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu "Ondoa" ondosha "ugumu" na ukali wa maradhi, "Ewe Mola wa watu" na Muumba wao na Mlezi wao, "na ponya" maradhi haya "wewe" Mtukufu "Ndiye mponyaji" na ninaomba kupitia jina lako Mponyaji, "hakuna ponyo" linaloweza kupatikana kwa mgonjwa "isipokuwa ponyo lako" na afya yako, "ponyo" la moja kwa moja "lisiloacha" na kubakisha na kuacha "ugonjwa" na maradhi mengine.

Faida

  • Mponyaji ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na daktari na dawa hivyo vyote ni sababu, havinufaishi wala havidhuru isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  • Kumtembelea mgonjwa ni katika haki zilizoko baina ya waislamu, nayo kwa familia inakuwa ni haki zaidi.
  • Himizo kwa mwenye kumtembelea mgonjwa amuombee dua hii yenye baraka na iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kujitibu kwa kisomo (cha Ruqya) ya kisheria kwa Qur'ani na dua nzuri, alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akijisomea mwenyewe anapougua, na vile vile alikuwa akimsomea yeyote mwenye kuhisi maumivu katika familia yake na watu wengine pia.
  • Amesema bin Hajari: Na imewatatiza baadhi ya watu dua ya kumuombea mgonjwa kupona hali yakuwa katika maradhi kuna kufutiwa madhambi na kupata thawabu kama zilivyokuja hadithi kwa wingi kuhusu hilo, na jawabu la hilo: Nikuwa dua ni ibada, na wala haiondoi thawabu na kufutiwa makosa; kwa sababu hayo hupatikana mwanzoni mwa ugonjwa na pale mtu anaposubiri juu ya maradhi, na muombaji anakuwa kati ya neema mbili: Ima apate lengo lake, au apewe badala kwa kuletewa manufaa au kuzuiliwa madhara, na yote hayo ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya mgonjwa: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Kihesabu kinafanyaje kazi?

Gusa kihesabu chini ya dhikri na kitahesabu kurudi nyuma hadi sifuri. Kipo kwenye ukurasa huu tu na hakuna kinachohifadhiwa.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.