Dua kabla ya kula (Bismillah)

Unachosema kabla ya chakula, na kwa nini jina la Allah hutajwa juu ya chakula.

1 Mara moja

بِسْمِ اللَّهِ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa kijana mdogo ndani ya nyumba ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na mkono wangu ulikuwa ukizunguka huku na kule katika sahani (ya chakula), akasema kuniambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kile kinachokuelekea" Ulibakia kuwa ndio ulaji wangu huo hata baada yake.

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Anaeleza Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-, huyu ni mtoto wa mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ummu Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na alikuwa chini ya malezi yake na usimamizi wake, kwamba yeye alikuwa wakati wa kula akihamisha mkono wake katika pande zote za chombo ili achukue chakula, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamfundisha adabu tatu miongoni mwa adabu za kula.

Adabu ya kwanza: Kusema: "Bismillah" Mwanzo wa kula.

Ya pili: Kula kwa mkono wa kulia.

Ya tatu: Kula upande ulio karibu naye katika chakula.

Faida

  • Katika adabu za kula na kunywa ni kusema Bismillahi mwanzo wake.
  • Kuwafundisha adabu watoto, hasa hasa wale walio chini ya malezi ya mtu.
  • Upole wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ameuonyesha katika kuwafundisha watoto na kuwaadabisha.
  • Katika adabu za chakula ni mtu kula kile kinachomuelekea, isipokuwa chakula kikiwa na aina tofauti tofauti, hapo anaruhusiwa kuchukua.
  • Masahaba kushikamana na yale aliyowaadabisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hili tunajifunza kutoka katika kauli ya Omari: Uliendelea kuwa ndio ulaji wangu hata baada yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho".

Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Ni nzuri (Hasan)

Maelezo

Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.

Faida

  • Kukusanyika kwa ajili ya chakula na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula ni sababu ya kupata baraka katika chakula, na kupatikana shibe kwa kukila kwake.
  • Utengano wote ni shari, na umoja wote ni heri.
  • Himizo la kukusanyika na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa chakula.
  • Amesema Assanadi: Kwa sababu ya mkusanyika baraka huteremka katika chakula, na kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Shetani hushindwa kukifikia chakula.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tunapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hatuweki mikono yetu mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi anaweka mkono wake, na hakika sisi kuna wakati tulihudhuria chakula pamoja naye, akaja kijakazi kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akamshika mkono wake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho, na bila shaka alikuja na kijakazi huyu ili akihalalishe, nikashika mkono wake, akaja tena na Bedui huyu ili akihalalishe nikamshika mkono, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wake umekamatwa na mkononi wangu pamoja na mkono wake kijakazi".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Hudhaifa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wanapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawaweki mikoni yao katika chakula mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka mkono wake, na hakika sisi tulihudhuria pamoja naye siku moja katika chakula, akaja kijakazi mmoja, kutokana na kasi yake kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kana kwamba anasukubwa, akamshika mkono wake kabla hajagusa chakula, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika Shetani hupata uwezo wa kula chakula, atakapoanza mtu kula chakula pasina kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuja na kijakazi huyu ili ajihalalishie kula, nikamshika mkono wake, kisha akaja na huyu Bedui, ili akihalalishe nikamshika mkono wake, ninamuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wa Shetani ulikuwa mkononi mwangu pamoja na mkono wake, kisha akataja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na akala.

Faida

  • Heshima ya Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na adabu yao kwake.
  • Katika adabu za chakula ni mdogo kusubiri mpaka aanze mkubwa na mwenye heshima katika kula.
  • Shetani huwasukuma baadhi ya watu wanaojisahau katika matendo ambayo yeye anayapenda; ili aweze kufikia lengo lake, na miongoni mwake ni haya yaliyoko katika hadithi hii.
  • Anasema Nawawi: Wanasema Wanachuoni: Na inapendeza mtu kutamka kwa sauti Bismillaah ili mwenzake asikie na amzindue kwa hilo.
  • Nikuwa atakapokuja mtu anataka kula na ukawa hujamsikia anasema Bismillaah basi mshike mkono wake mpaka aseme Bismillaah.
  • Uwajibu wa kuondoa uovu kwa mwenye kujua, na kuondoa uovu kwa mkono kwa mwenye uwezo.
  • Hadithi hii ni alama niongoni mwa alama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjulisha kilichotokea katika kisa hiki.
  • Shetani hapati uwezo wa kula chakula cha watu wenye imani isipokuwa kama wasipotaja jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho.
  • Inapendeza kuwafundisha watu adabu za kula na kunywa katika Uislamu.
  • Inapendeza kutoa kiapo; kwa ajili ya kusisitiza jambo kwa msikilizaji.
  • Amesema Nawawi: Bismillaah wakati wa kunywa maji na maziwa na Asali na mchuzi na dawa na vinywaji vinginevyo ni kama Bismillaah wakati wa chakula.
  • Amesema Nawawi: Na ikiwa mtu ataacha Bismillaah mwanzo wa chakula kwa makusudi au kwa kusahau au kwa ujinga au kwa kulazimishwa au kwa kushindwa kwa sababu yoyote ile iliyojitokeza, kisha akaweza kufanya hivyo wakati wa kula kwake, basi ni sunna aseme: "Bismillaahi Awwalihi wa Aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Akatapokula mmoja wenu basi na ataje jina la Mwenyezi Mungu, na ikiwa atasahau kumtaja Mwenyezi Mungu mwanzo wa chakula, basi na aseme: Bismillaahi Awwalihi Wa Aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake". Kaipokea Abuu Daudi na Tirmidhi.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

Maana na chanzo

ImepokelewaKutoka kwa Jabir radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku, na anapoingia na hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake, Shetani husema: Mmepata malazi, na asipomtaja Mwenyezi Mungu wakati wa chakula chake, husema: Mmepata malazi na chakula cha usiku".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtaja Allah wakati wa kuingia nyumbani na kabla ya kupata chakula, nakuwa mtu akimtaja Mwenyezi Mungu kwa kusema: (Bismillaah) -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- wakati wa kuingia nyumbani kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema kuwaambia wasaidizi wake: Hamna bahati leo ya kupata malazi wala chakula cha usiku ndani ya nyumba hii ambayo mwenye nyumba kajilinda kutokana nanyi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ama mtu akiingia nyumbani kwake na akawa hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake wala wakati wa kupata kwake chakula, Shetani huwaeleza wasaidizi wake kuwa wamepata mahali pa kulala, na chakula cha usiku ndani ya nyumba hii.

Faida

  • Ni sunna kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia nyumbani na wakati wa chakula, kwani Shetani hulala ndani ya majumba, na hula katika chakula cha wenye nyumba ikiwa hawatomtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Shetani humfuatilia mwanadamu katika matendo yake na harakati zake na katika mambo yake yote, akijisahau kumtaja Allah papo hapo hupata lengo lake kwake.
  • Kumtaja Allah humfukuza Shetani.
  • Kila Shetani anawafuasi na ana vipenzi ambao huchukua ushauri wake na kufuata amri yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua kabla ya kula: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.