Somo la 5 kati ya 5
Hija ni nini?
Kutoka Kurani
إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٖ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكٗا وَهُدٗى لِّلۡعَٰلَمِينَ ﴿٩٦﴾ فِيهِ ءَايَٰتُۢ بَيِّنَٰتٞ مَّقَامُ إِبۡرَٰهِيمَۖ وَمَن دَخَلَهُۥ كَانَ ءَامِنٗاۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلٗاۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴿٩٧﴾
Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, (Makka) iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote. Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.
وَأَذِّن فِي ٱلنَّاسِ بِٱلۡحَجِّ يَأۡتُوكَ رِجَالٗا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٖ يَأۡتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٖ ﴿٢٧﴾
Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.
Kutoka Sunna
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.
Safari imekamilika
Hongera!
Nguzo tano za Uislamu
Safari 1 kati ya 6 zimekamilika
Anza safari inayofuataImani ya Waislamu