Swala ya jeneza: jinsi ya kuiswali

Swala ya jeneza hatua kwa hatua, pamoja na dua zake na hadithi inazotokana nazo.

Jinsi inavyoswaliwa

  1. Simama ukielekea Qibla, nyuma ya maiti, kwa nia ya swala ya jeneza. Sema takbira ya kwanza (Allahu akbar) na usome al-Fatiha.
  2. Sema takbira ya pili, kisha umswalie Mtume ﷺ kama katika tashahhud.
  3. Sema takbira ya tatu, kisha umwombee dua maiti.
  4. Sema takbira ya nne, simama kidogo, kisha umalize swala kwa salamu.

Hakuna rukuu, hakuna sijda, hakuna adhana wala iqama. Katika madhehebu ya Hanafi, sifa ya kufungua (thanaa) husomwa baada ya takbira ya kwanza badala ya al-Fatiha.

Hadithi

1 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwenda mbio kuliandaa jeneza na kuliswalia na kuzika; jeneza likiwa jema basi mnaliwahisha kwenda katika kheri miongoni mwa neema za kaburi, na likiwa kinyuume na hivyo, basi hiyo ni shari mnaiweka katika shingo zenu.

Faida

  • Amesema bin Hajari: Inapendeza na ni sunna kwenda haraka, lakini kwa kiwango ambacho si cha nguvu, kiasi ambacho yanaweza kuhofiwa madhara kwa maiti, au uzito kwa mbebaji au msindikizaji.
  • Hapa kuna mpaka katika uharaka, ni pale ikiwa kifo kitakuwa cha ghafla, kwani inahofiwa inaweza kuwa ni kuzimia tu, hapa ni inatakiwa asizikwe ila baada ya kuthibitsha kifo chake, au inaweza kuwa kuchelewesha kidogo kwa ni kwa sababu ya masilahi, kama kuongezeka wa kumswalia, au kuhudhuria ndugu zake wa karibu, endapo hatohofiwa kuharibika.
  • Himizo la kulipeleka haraka jeneza ni kwa ajili ya masilahi ya maiti akiwa ni mtu mwema, au kwa ajili ya masilahi ya wasindikizaji akiwa ni mtu muovu.
  • Amesema Nawawi: Na inachukuliwa faida hapa kuwa mtu aache kusuhubiana na watu waovu wasiokuwa wema.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Anatuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Tuseme na turudie neno la kumpwekesha "Laa ilaah illa llaah" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kufikwa kwake na tabu za kifo mpaka aliseme, ili liwe neno lake la mwisho.

Faida

  • Sunna ya kumtamkisha aliyefikwa na mauti.
  • Inachukiza kukariri sana kumtamkisha aliyefikwa na umauti, na kumlazimisha endapo atalitamka, au ikafahamika kuwa ametamka; ili wasimsumbue akatamka maneno yasiyofaa.
  • Amesema Nawawi: Na akilitamka mara moja basi asilikariri tena isipokuwa kama atatamka baada yake maneno mengine, hapo litarudiwa tena ili liwe neno lake la mwisho.
  • Hadithi inakusanya kuhudhuria mbele ya aliyefikwa na umauti ili kumkumbusha na kumliwaza na kumfunga macho na kusimamia haki zake.
  • Si sheria kumtamkisha mtu baada ya kifo na kaburini baada ya mazishi; kwa sababu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutolifanya hilo.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Swala ya jeneza: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.