Ruqya kutoka Sunna: dua za maumivu na kupona

Maneno ya kuponya aliyotumia na kufundisha Mtume ﷺ.

1 Mara moja

بِاسْمِ اللهِ (٣)
أَعُوذُ بِاللهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ (٧)

Maana na chanzo

Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi Ath-thaqafi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maumivu anayoyapata katika mwili wake tangu aliposilimu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)"

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Othman bin Abil Aswi alipata maumivu makali ambayo yalikaribia kumuua, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaenda kumtembelea, na akamfundisha dua ambayo Mwenyezi Mungu atamuondolea maradhi yaliyomfika; nayo ni aweke mkono wake juu ya mahala panapoumia, na aseme: "Bismillaah" mara tatu, kisha aseme mara saba: "Ninataka kinga" na ninajikinga na kujiweka na kujilinda (kwa Mwenyezi Mungu na kudura zake kutokana na shari za yale ninayoyapata) katika maumivu ya wakati huu (na kuyahofia) na ninahofia kutokea maumivu mengine baadaye miongoni mwa huzuni na hofu, au kuendelea kwa maradhi na yakasambaa maumivu yake katika mwili.

Faida

  • Sunna ya mtu kujifanyia kisomo cha ruqya yeye mwenyewe kama ilivyokuja katika hadithi.
  • Malalamiko -pasina kuchukizwa na hali wala kupingana na Kadari- hakupingani na kutawakali na subira.
  • Dua ni miongoni mwa kuchukua sababu, na ndio maana ni lazima kushikamana na matamshi yake na idadi yake.
  • Dua hii inasomwa kwa maumivu ya kila kiungo.
  • Kuweka mkono juu ya mahala palipo na maumivu wakati wa kusoma dua hii.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِدٍ، اللهُ يَشْفِيكَ بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Jibril alimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Muhammad umetekesa kwa maumivu? Akasema: "Ndiyo" Akasema: "Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea.

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuja Malaika Jibril amani iwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamuuliza: Ewe Muhammad, unalalamika kwa maradhi? Akasema: Ndiyo. Jibril akamsomea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa kusema: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu" Kwa kutaka msaada kwa jina hilo "Ninakusomea" na ninakukinga, "kutokana na kila kitu kinachokuudhi" Kiwe kikubwa au kidogo, "kutokana na shari ya kila nafsi" chafu, "au jicho la hasidi" lisije kukufika, basi Mwenyezi Mungu "atakuponya" na akukinge na akuhifahdi dhidi ya kila maradhi, "kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea" amelikariri neno hili kwa ajili ya ziada, na ameanza nalo na amemaliza nalo akiashiria kuwa hakuna awezaye kunufaisha isipokuwa Yeye Mtukufu.

Faida

  • Kufaa kuelezea maradhi ikiwa kama ni kuelezea uhalisia wa hali, na si sehemu ya kunung'unika na kulalamika.
  • Inafaa kusoma Ruqya kwa sharti zifuatazo: 1- Iwe kwa Qur'ani au kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na dua za kisheria. 2- Iwe kwa lugha ya kiarabu, au kwa maneno yanayoeleweka maana yake katika lugha zingine. 3- Aamini kuwa Ruqya haiathiri yenyewe; bali ni sababu miongoni mwa sababu, haina athari yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. 4- Iiepukane na ushirikina, au haramu, au uzushi, au yenye kupelekea katika hayo.
  • Kumethibitishwa madhara ya kijicho, na kwamba ni kweli, inatakiwa kujisomea kutokana na kijicho.
  • Ni sunna kujifanyia kisomo kupitia yale yaliyokuja katika hadithi.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kama watu wengine, humtokea yale yanayowatokea watu wengine, kama maradhi.
  • Ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake na kumuhifadhi kwake, na kumuwekea kwake Malaika kwa ajili ya hilo.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Ruqya kutoka Sunna: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.