Dua ya kuingia na kutoka chooni

Unachosema kabla ya kuingia chooni na baada ya kutoka.

1 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الخُبُثِ وَالخَبَائِثِ

Maana na chanzo

Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia mahali ambapo atakidhi haja yake hapo, haja ndogo au kubwa, anaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu, na anajielekeza kwake amkinge na shari za mashetani wa kiume na wa kike, Na limetafsiriwa neno khubuthi na khabaaithi (Mashetani wa kiume na wa kike) kwa maana ya shari na najisi.

Faida

  • Sunna ya dua hii wakati wa kutaka kuingia msalani.
  • Viumbe wote ni wahitaji kwa Mola wao Mlezi katika kuzuia yenye kuwaudhi au kuwadhuru katika hali zao zote.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

غُفْرَانَكَ

Maana na chanzo

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotoka kukidhi haja yake msalani anasema: " Ninakuomba (Msamaha) Ewe Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Ni sunna kusema: "Ghufraanaka" baada ya kutoka mahala pa kukidhi haja.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumtaka msamaha Mola wake katika hali zake zote.
  • Inasemekana katika sababu ya kuomba msamaha baada ya kukidhi haja ni kwa sababu ya uzembe wa kushukuru neema nyingi za Mwenyezi Mungu, ikiwemo kurahisishiwa kutoka kile kinachokuudhi, na ninaomba msamaha wako kwa kushughulishwa na kukidhi haja nikaacha kukutaja.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya chooni: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.