Last ten ayahs of Al-Kahf

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

ٱلَّذِينَ كَانَتۡ أَعۡيُنُهُمۡ فِي غِطَآءٍ عَن ذِكۡرِي وَكَانُواْ لَا يَسۡتَطِيعُونَ سَمۡعًا ١٠١

Alladhīna kānat a'yunuhum fī ghitā'in 'an dhikrī wakānū lā yastatī'ūna sam'ā

Wale ambao kwamba macho yao yalikuwa paziani hayanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia. 101

Maelezo ya chini

101 Na hayo ni kwa kuwa macho yao walipo kuwa duniani yalikuwa yameghafilika hayaoni Ishara za Mwenyezi Mungu kama kwamba yamezibwa na pazia; na walikuwa kwa upotovu wao hawawezi kusikia Wito wa Haki, kama mtu aliye kuwa kiziwi. "Wale ambao kwamba macho yao yalikuwa paziani hayanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia": Ni wale ambao macho yao yameghafilika na kunizingatia Mimi katika mbingu na ardhi. Na kwa hivyo hii Aya tukufu inazindua watu wazingatie yote yalio wazunguka yanayo onyesha Ishara za kuwepo Mwenyezi Mungu.

أَفَحَسِبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن يَتَّخِذُواْ عِبَادِي مِن دُونِيٓ أَوۡلِيَآءَۚ إِنَّآ أَعۡتَدۡنَا جَهَنَّمَ لِلۡكَٰفِرِينَ نُزُلٗا ١٠٢

Afahasibal-ladhīna kafarū an yattakhidhū 'ibādī min dūnī awliyā'a innā a'tadnā jahannama lil-kāfirīna nuzulā

Je, wanadhani walio kufuru ndio wawafanye waja wangu ndio walinzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo mahala pa kuteremkia makafiri. 102

Maelezo ya chini

102 Je, macho ya makafiri yamepofuka hata wakadhani kwamba kuwafanya watumwa wangu, Malaika na Isa, kuwa ni miungu, wakiwaabudu badala yangu Mimi, kutawapa manufaa na kuwakinga na adhabu? Hakika Sisi tumewaandalia Jahannamu ndio pahali pao pa kukaa wapate huko malipo wanayo yastahiki.

قُلۡ هَلۡ نُنَبِّئُكُم بِٱلۡأَخۡسَرِينَ أَعۡمَٰلًا ١٠٣

Qul hal nunabbi'ukum bil-akhsarīna a'mālā

Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao?. 103

Maelezo ya chini

103 Ewe Mtume! Waambie hawa makafiri: Je, nikutajieni watu watao pata khasara mno kwa vitendo vyao na watao kosa thawabu?

ٱلَّذِينَ ضَلَّ سَعۡيُهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُمۡ يَحۡسَبُونَ أَنَّهُمۡ يُحۡسِنُونَ صُنۡعًا ١٠٤

Alladhīna dalla sa'yuhum fil-hayawātid-dunyā wahum yahsabūna annahum yuhsinūna sun'ā

Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri. 104

Maelezo ya chini

104 Ni hao vilio haribika vitendo vyao katika maisha ya duniani kwa kuharibika itikadi yao, na hali wao wanaitakidi kuwa ndio wanafanya vitendo vyema!

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ وَلِقَآئِهِۦ فَحَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَلَا نُقِيمُ لَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَزۡنٗا ١٠٥

Ulā'ikal-ladhīna kafarū bi'āyāti rabbihim waliqā'ihī fahabitat a'māluhum falā nuqīmu lahum yawmal-qiyāmati waznā

Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawathamini kitu. 105

Maelezo ya chini

105 Hao ndio walio zikataa dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu, na wakaikanusha Siku ya kufufuliwa na kuhisabiwa. Basi vitendo vyao vimepotea bure, na Siku ya Kiyama watastahiki kudharauliwa na kupuuzwa, kwani hawana a'mali ya kutiwa maanani!

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُمۡ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُواْ وَٱتَّخَذُوٓاْ ءَايَٰتِي وَرُسُلِي هُزُوًا ١٠٦

Dhālika jazā'uhum jahannamu bimā kafarū wattakhadhū āyātī warusulī huzuwā

Hiyo Jahannamu ni malipo yao kwa walivyo kufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu. 106

Maelezo ya chini

106 Hayo ndiyo tuliyo yabainisha na tukayapambanua, hali ya hawa; na malipo yao kwa hayo ni Jahannamu kwa sababu ya kufuru zao na kuzifanyia maskhara Ishara za Mwenyezi Mungu alizo ziteremsha, na Mitume alio watuma.

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ كَانَتۡ لَهُمۡ جَنَّٰتُ ٱلۡفِرۡدَوۡسِ نُزُلًا ١٠٧

Innal-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti kānat lahum jannātul-firdawsi nuzulā

Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. 107

Maelezo ya chini

107 Hakika walio thibiti katika Imani na wakatenda mema, malipo yao ni Bustani za Firdausi watazo ziingia.

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يَبۡغُونَ عَنۡهَا حِوَلٗا ١٠٨

Khālidīna fīhā lā yabghūna 'anhā hiwalā

Watadumu humo; hawatataka kuondoka. 108

Maelezo ya chini

108 Wataneemeka milele, wala hawatataka badala yake chochote.

قُل لَّوۡ كَانَ ٱلۡبَحۡرُ مِدَادٗا لِّكَلِمَٰتِ رَبِّي لَنَفِدَ ٱلۡبَحۡرُ قَبۡلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَٰتُ رَبِّي وَلَوۡ جِئۡنَا بِمِثۡلِهِۦ مَدَدٗا ١٠٩

Qul law kānal-bahru midādal likalimāti rabbī lanafidal-bahru qabla an tanfada kalimātu rabbī walaw ji'nā bimithlihī madadā

Sema: Lau kuwa bahari ndio wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea. 109

Maelezo ya chini

109 Ewe Mtume! Waambie watu: Hakika ujuzi wa Mwenyezi Mungu umekusanya kila kitu. Na lau kuwa maji ya baharini ni wino wa kuandikia maneno ya Mwenyezi Mungu yanayo onyesha ujuzi wake na hikima yake, basi wino huo ungeli malizika, na hata ungeli ongezwa wino mwingine kama huo, kabla ya kumalizika maneno ya Mwenyezi Mungu!

قُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يُوحَىٰٓ إِلَيَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ فَمَن كَانَ يَرۡجُواْ لِقَآءَ رَبِّهِۦ فَلۡيَعۡمَلۡ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَلَا يُشۡرِكۡ بِعِبَادَةِ رَبِّهِۦٓ أَحَدَۢا ١١٠

Qul innamā ana basharum mithlukum yūhā ilayya annamā ilāhukum ilāhun wāhidun faman kāna yarjū liqā'a rabbihī falya'mal 'amalan sālihan walā yushrik bi'ibādati rabbihī ahadā

Sema: Mimi ni mwanaadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi. 110

Maelezo ya chini

110 Ewe Mtume! Waambie watu: Hakika mimi ni mtu tu kama nyinyi, nimetumwa kwenu, nikufunzeni aliyo nifunza Mwenyezi Mungu. Nimefunuliwa (yaani nimepewa Wahyi) ya kwamba Mungu wenu ni Mmoja, hana mshirika wake. Anaye tumai kukutana na Mwenyezi Mungu na kupata malipwa yake, basi naatende vitendo vyema kwa usafi wa niya, na ajitenge mbali na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote katika ibada.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Kahf yote

Maswali

Last ten ayahs of Al-Kahf iko wapi katika Qur'ani?

Last ten ayahs of Al-Kahf iko katika Surat Al-Kahf, 18:101-110.