Surat At-Tawbah, aya 118

9:118

وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُواْ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ وَضَاقَتۡ عَلَيۡهِمۡ أَنفُسُهُمۡ وَظَنُّوٓاْ أَن لَّا مَلۡجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيۡهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡ لِيَتُوبُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ ١١٨

Wa'alath-thalāthatil-ladhīna khullifū hattā idhā dāqat 'alayhimul-ardu bimā rahubat wadāqat 'alayhim anfusuhum wazannū al lā malja'a minallāhi illā ilayhi thumma tāba 'alayhim liyatūbū innallāha huwat-tawwābur-rahīm

Na pia wale watatu walio achwa nyuma hata dunia wakaiona dhiki juu ya ukunjufu wake, na nafsi zao zikabanika, na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu. 118

Maelezo ya chini

118 Na pia Mwenyezi Mungu aliwafadhili wale wanaume watatu walio baki nyuma wasitoke kwenda kwenye Jihadi katika vita vya Tabuk. Hawa hawakubaki nyuma kwa unaafiki. Ilikuwa inatarajiwa Mwenyezi Mungu atoe bayana ya hukumu yao. Ilivyo kuwa toba yao ni ya kweli, na majuto yao makubwa hata wakaiona dunia nyembamba juu ya upana wake, na nafsi zao zikaingiwa na dhiki kwa hamu na huzuni, na wakajua kuwa hapana pa kuikimbia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa kumwomba Yeye msamaha na kurejea kwake. Hapo basi Mwenyezi Mungu aliwaongoa watubu. Na Yeye akawasamehe, ili wapate kuendelea na hali ya toba. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba za wenye kutubu, ni Mwingi wa kuwarehemu waja wake.