وَكَذَٰلِكَ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ رُوحٗا مِّنۡ أَمۡرِنَاۚ مَا كُنتَ تَدۡرِي مَا ٱلۡكِتَٰبُ وَلَا ٱلۡإِيمَٰنُ وَلَٰكِن جَعَلۡنَٰهُ نُورٗا نَّهۡدِي بِهِۦ مَن نَّشَآءُ مِنۡ عِبَادِنَاۚ وَإِنَّكَ لَتَهۡدِيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ ٥٢
Wakadhālika awhaynā ilayka rūham min amrinā mā kunta tadrī mal-kitābu walal-īmānu walākin ja'alnāhu nūran nahdī bihī man nashā'u min 'ibādinā wa innaka latahdī ilā sirātim mustaqīm
Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. 52
Maelezo ya chini
52 Na kama tulivyo wafunulia Mitume kabla yako, basi tumekufunulia nawe, ewe Mtume, hii Qur'ani ili ihuishe nyoyo kwa amri yetu. Kabla ya kuletewa wewe hii ulikuwa hujui nini Qur'ani, wala hujui Sharia za Imani. Lakini tumeifanya Qur'ani kuwa ni Nuru Kubwa ya kuwaongoza wenye kukhiari Uwongofu. Na wewe bila ya shaka utakuwa ukiwaitia watu kwa hii Qur'ani kwenye Njia Iliyo Nyooka.