۞ وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ ٱللَّهُ إِلَّا وَحۡيًا أَوۡ مِن وَرَآيِٕ حِجَابٍ أَوۡ يُرۡسِلَ رَسُولٗا فَيُوحِيَ بِإِذۡنِهِۦ مَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ عَلِيٌّ حَكِيمٞ ٥١
Wamā kāna libasharin an yukallimahullāhu illā wahyan aw min warāy'i hijābin aw yursila rasūlan fayūhiya bi idhnihī mā yashā'u innahū 'aliyyun hakīm
Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima. 51
Maelezo ya chini
51 Wala haimfalii mtu kusemezwa na Mwenyezi Mungu ila iwe kwa Wahyi (Ufunuo) kwa kumtilia ilhamu katika moyo wake, au usingizini, au kwa kusikia maneno ya Kiungu bila ya kumwona Asemaye, au kwa kutumwa Malaika akaonekana sura yake, na akasikilizana sauti, akamfunulia Nabii kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama atakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtenda nguvu, basi haziwiliki Mwenye kupita ukomo hikima yake katika kuendesha mambo yake na kupanga kwake.