Surat An-Nisa, aya 142

4:142

إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمۡ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلٗا ١٤٢

Innal-munāfiqīna yukhādi'ūnallāha wahuwa khādi'uhum wa idhā qāmū ilas-salawāti qāmū kusālā yurā'ūnan-nāsa walā yadhkurūnallāha illā qalīlā

Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kuswali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu. 142

Maelezo ya chini

142 Hakika wanaafiki, kwa ule unaafiki wao, wanadhani kuwa wanamkhadaa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wanamficha hakika ya nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Yeye ndiye anaye wakhadaa wao. Basi Yeye huwapururia kuwapa muhula, na anawawacha mpaka wabobee katika maovu yao, kisha ndio awahisabu kwa waliyo yatenda. Na hawa wanaafiki wana dhaahiri ya kuonekana, na ya ndani ya nafsi zao. Yale ya kuonekana ni vile kuwa wakiinuka kwenda kuswali huinuka kwa uvivu, kwa unyong'onyo. Na Swala yao ni riya tu, kuonyesha, si ya kweli. Na ya ndani ni kuwa hawakumbuki kumtaja Mwenyezi Mungu ila kwa nadra, kwa tukizi. Na lau kuwa wanamkumbuka vilivyo wangeli uacha unaafiki