ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا ١٤١
Alladhīna yatarabbasūna bikum fa in kāna lakum fathum minallāhi qālū alam nakum ma'akum wa in kāna lil-kāfirīna nasībun qālū alam nastahwidh 'alaykum wanamna'kum minal-mu'minīna fallāhu yahkumu baynakum yawmal-qiyāmati walan yaj'alallāhu lil-kāfirīna 'alal-mu'minīna sabīlā
Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini. 141
Maelezo ya chini
141 Mtindo wa wanaafiki ni kukungojeeni kama anavyo ngojea mwenye husda na maya anaye tamani mpate masaibu mnapo kuwa katika vita na maadui. Mkishinda kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, na mkafungukiwa njia ya Haki, wao huwaambia Waumini - na hali wao ule ushindi walio pewa wenye Imani na Mwenyezi Mungu umewashtusha : Sisi hatukuwa nanyi? Kwa maana sisi ni jamaa zenu! Na ikiwa ni zamu ya makafiri kupata ushindi, basi wao huwaendea na kuwaambia: Sisi hatukuyashughulikia mambo yenu hata yakawa ni yetu? Na hatukukupeni mapenzi yetu, na tukakulindeni na hawa Waumini? (yaani sisi ni wenzenu). Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la atakuhukumuni baina yenu na hawa wanaafiki Siku ya Kiyama. Wala Mwenyezi Mungu hatowapa makafiri njia kuwashinda Waumini maadamu Waumini watashikamana na sifa ya Imani ya kweli na vitendo vyema.