مُّذَبۡذَبِينَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا ١٤٣
Mmudhabdhabīna bayna dhālika lā ilā hā'ulā'i walā ilā hā'ulā'i waman yudlilillāhu falan tajida lahū sabīlā
Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako na huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, kabisa hutompatia njia. 143
Maelezo ya chini
143 Na hawa wanaafiki ni watu wanao taradadi, wanababaika. Kwenu hawapo, na kwao makafiri hawapo katika kila hali. Na hayo ni kwa sababu ya udhaifu wa imani, na udhaifu wa nafsi, na kwa sababu ya kupotoka na Haki. Na mwenye kuandikiwa kupotoka na Mwenyezi Mungu tangu hapo azali, basi huna njia wewe ya kumwongoa sawa.