Surat Al-Imran, aya 165

3:165

أَوَلَمَّآ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَدۡ أَصَبۡتُم مِّثۡلَيۡهَا قُلۡتُمۡ أَنَّىٰ هَٰذَاۖ قُلۡ هُوَ مِنۡ عِندِ أَنفُسِكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ١٦٥

Awalammā asābatkum musībatun qad asabtum mithlayhā qultum annā hādhā qul huwa min 'indi anfusikum innallāha 'alā kulli shay'in qadīr

Nyinyi - ulipo kusibuni msiba ambao nyinyi mmekwisha watia mara mbili mfano wa huo - mnasema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo umetoka kwenu wenyewe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. 165

Maelezo ya chini

165 Hivyo mnapigwa na mshangao na kuemewa pale yalipo kupateni siku ya Uhud masaibu ambayo nyinyi mlikwisha wapa maadui mara mbili mfano wa hayo katika siku ya Badri, hata mnasema kwa mastaajabu: Yamekuwaje mauwaji haya na kushindwa huku, na sisi ni Waislamu na Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nasi? Sema: Yaliyo kupateni yametokana na nafsi zenu kwa vile mlivyo mkhalifu Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, naye amekulipeni kwa mujibu wa mlivyo tenda.