وَمَآ أَصَٰبَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ فَبِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٦٦
Wamā asābakum yawmal-taqal-jam'āni fabi'idhnillāhi waliya'lamal-mu'minīn
Na yaliyo kusibuni siku yalipo pambana majeshi mawili yalikuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awajue Waumini. 166
Maelezo ya chini
166 Enyi Waumini! Yaliyo kusibuni lilipo pambana jeshi lenu na jeshi la Washirikina katika Uhud yametokana kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu, na ili awadhihirishie watu Imani ya Waumini ya kweli aliyo ifunza.