Surat Al-Baqarah, aya 97

2:97

قُلۡ مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّـجِبۡرِيلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلۡبِكَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ ٩٧

Qul man kāna 'aduwwal lijibrīla fa innahū nazzalahū 'alā qalbika bi idhnillāhi musaddiqal limā bayna yadayhi wahudan wabushrā lil-mu'minīn

Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini. 97

Maelezo ya chini

97 Na baadhi yao wanadai kuwa wanakupinga na wanakikataa Kitabu chako kwa kuwa ati wao ni maadui wa Jibril anaye kufikishia hichi Kitabu. Basi sema ewe Nabii uwaambie: Anaye kuwa Jibril ni adui wake, basi vile vile huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu Jibril haji na Kitabu hichi kwa nafsi yake, bali anakiteremsha kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na Kitabu hichi kinathibitisha Vitabu vilivyo tangulia kutoka mbinguni.. na kinathibitisha Kitabu chenu wenyewe..na hii Qur'ani (inayo teremshwa na Jibril kutoka kwa Mwenyezi Mungu) ni Uwongofu na Bishara njema kwa Waumini.