مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّلَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبۡرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوّٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ ٩٨
Man kāna 'aduwwa lillāhi wamalā'ikatihī warusulihī wajibrīla wamīkāla fa innallāha 'aduwwul lil-kāfirīn
Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri. 98
Maelezo ya chini
98 Basi yeyote anaye kuwa ni adui wa Jibril, au Mikail, au Malaika yeyote au Mtume yeyote, miongoni mwa Malaika na Mitume wa Mwenyezi Mungu, ambao hawafanyi kitu wala hawapeleki ujumbe ila kama vile Mwenyezi Mungu anavyo waamrisha, basi mtu huyo anakuwa ni adui wa Mwenyezi Mungu, na anakuwa kafiri anamkataa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.