حَٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوَٰتِ وَٱلصَّلَوٰةِ ٱلۡوُسۡطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَٰنِتِينَ ٢٣٨
Hāfizū 'alas-salawāti was-salawātil-wustā waqūmū lillāhi qānitīn
Zilindeni Swala, na khasa Swala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea). 238
Maelezo ya chini
238 Fanyeni hima katika kusimamisha Swala zote na kuzidumisha. Na fanyeni hima kuwa Swala yenu iwe ni Swala bora kwa kuzitimiza nguzo zake na kumsafia niya Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu katika Swala. Na timizeni ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mkumbukeni kwa usafi wa moyo na kunyenyekea Utukufu wake.