Surat Al-Baqarah, aya 237

2:237

وَإِن طَلَّقۡتُمُوهُنَّ مِن قَبۡلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدۡ فَرَضۡتُمۡ لَهُنَّ فَرِيضَةٗ فَنِصۡفُ مَا فَرَضۡتُمۡ إِلَّآ أَن يَعۡفُونَ أَوۡ يَعۡفُوَاْ ٱلَّذِي بِيَدِهِۦ عُقۡدَةُ ٱلنِّكَاحِۚ وَأَن تَعۡفُوٓاْ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۚ وَلَا تَنسَوُاْ ٱلۡفَضۡلَ بَيۡنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ ٢٣٧

Wa in tallaqtumūhunna min qabli an tamassūhunna waqad faradtum lahunna farīdatan fanisfu mā faradtum illā an ya'fūna aw ya'fuwal-ladhī biyadihī 'uqdatun-nikāhi wa an ta'fū aqrabu lit-taqwā walā tansawul-fadla baynakum innallāha bimā ta'malūna basīr

Na mkiwapa T'alaka kabla ya kuwagusa, na mmekwisha wawekea hayo mahari makhsusi, basi wapeni nusu ya mahari mlio agana, isipo kuwa ikiwa wanawake wenyewe wamesamehe, au mume ambaye kifungo cha ndoa ki mikononi mwake awe amesamehe. Na kusameheana ndiko kulio karibu zaidi na uchamngu. Wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. 237

Maelezo ya chini

237 Pindi mkiwapa T'alaka wanawake kabla ya kuingia harusi lakini baada ya kwisha wafikiana mahari, basi ni haki yao hao wat'alaka wapewe nusu ya mahari, ila wenyewe kwa ridhaa yao wakikataa kuchukua kitu. Na wao pia hawapewi zaidi ya nusu ila waume nafsi zao wakasamehe na wakatoa mahari yote kaamili. Na kila mmoja wapo kusamehe ndio ubora zaidi na ni kumridhisha zaidi Mwenyezi Mungu, na ndio mambo yanavyo elekea kwa wachao Mungu. Basi msiache huu mwendo wa kusameheana. Na kumbukeni kuwa kheri iko katika kufadhiliana na kufanyiana ihsani. Hayo ndiyo yanayo pelekea kupendana baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema dhamiri zenu na atakulipeni kwa fadhila mzitendazo.