Surat Al-Baqarah, aya 239

2:239

فَإِنۡ خِفۡتُمۡ فَرِجَالًا أَوۡ رُكۡبَانٗاۖ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ ٢٣٩

Fa in khiftum farijālan aw rukbānan fa idhā amintum fadhkurullāha kamā 'allamakum mā lam takūnū ta'lamūn

Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapo kuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyo kufunzeni yale mliyo kuwa hamyajui. 239

Maelezo ya chini

239 Ukikufikieni wakati wa Swala nanyi mko katika khofu basi msiache kusali, bali swalini kama muwezavyo, ikiwa huku mnakwenda kwa miguu au mmepanda kipando. Ikiondoka khofu swalini kwa kutimiza nguzo zote kama mlivyo jifunza, mkimkumbuka Mwenyezi Mungu katika Swala na mkimshukuru kwa aliyo kufunzeni, na kwa kukujaalieni kuwa katika amani.