ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ وَهِيَ دُخَانٞ فَقَالَ لَهَا وَلِلۡأَرۡضِ ٱئۡتِيَا طَوۡعًا أَوۡ كَرۡهٗا قَالَتَآ أَتَيۡنَا طَآئِعِينَ ١١
Thummastawā ilas-samā'i wahiya dukhānun faqāla lahā walil-ardi'tiyā taw'an aw karhan qālatā ataynā tā'i'īn
Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu. 11
Maelezo ya chini
11 Kisha amekhusisha uweza wake na kuumba mbingu, nazo zilikuwa kama moshi, basi zikawapo. Na kuumba kwake mbingu na ardhi kwa mujibu wa mapendo yake ni jambo jepesi kwake, ni kama kukiambia kitu: Njoo ukipenda usipenda, nacho kikat'ii.