فَقَضَىٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَٰوَاتٖ فِي يَوۡمَيۡنِ وَأَوۡحَىٰ فِي كُلِّ سَمَآءٍ أَمۡرَهَاۚ وَزَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَٰبِيحَ وَحِفۡظٗاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ ١٢
Faqadāhunna sab'a samāwātin fī yawmayni wa awhā fī kulli samā'in amrahā wazayyannas-samā'ad-dunyā bimasābīha wahifzan dhālika taqdīrul-'azīzil-'alīm
Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua. 12
Maelezo ya chini
12 Na akatimiza kuumba mbingu saba mnamo siku mbili nyengine. Na akaweka katika kila mbingu alicho kiandalia na ilivyo pelekea hikima yake. Na akaipamba mbingu ya karibu na dunia kwa nyota zinazo ng'ara kama taa, kwa ajili ya uwongofu wasisikilize mashetani khabari za walio juu. Kuumba huko vilivyo ni mpango wa Mwenyezi Mungu asiye shindika, Mwenye kuzunguka kila kitu.