Surat Ash-Shura, aya 34

42:34

أَوۡ يُوبِقۡهُنَّ بِمَا كَسَبُواْ وَيَعۡفُ عَن كَثِيرٖ ٣٤

Aw yūbiqhunna bimā kasabū waya'fu 'an kathīr

Au huviangamiza hivyo vyombo kwa sababu ya waliyo yatenda hao watu. Naye husamehe mengi. 34

Maelezo ya chini

34 Au akayateketeza hayo majahazi kwa sababu ya madhambi ya walio panda, kwa kuwapelekea upepo wa kimbunga. Na Mwenyezi Mungu akipenda anasamehe mengi; kwa kuwa hawaadhibu kwa kuzuia upepo na kuleta shuwari, au kwa kuleta kimbunga cha kuwazamisha.