Surat Ash-Shura, aya 33

42:33

إِن يَشَأۡ يُسۡكِنِ ٱلرِّيحَ فَيَظۡلَلۡنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٍ ٣٣

In yasha' yuskinir-rīha fayazlalna rawākida 'alā zahrihī inna fī dhālika la'āyātil likulli sabbārin shakūr

Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru. 33

Maelezo ya chini

33 Mwenyezi Mungu akipenda huutuliza upepo kukawa shuwari; basi majahazi yaliyo thibiti juu ya bahari hutulia hayendi huko yendako. Hakika huko kwenda kwao na kusimama kwao kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni dalili wazi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu. Wanayazingatia hayo Waumini wenye kusubiri wakati wa dhiki, na wenye kushukuru wakati wa furaha.