Surat An-Nisa, aya 76

4:76

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱلطَّٰغُوتِ فَقَٰتِلُوٓاْ أَوۡلِيَآءَ ٱلشَّيۡطَٰنِۖ إِنَّ كَيۡدَ ٱلشَّيۡطَٰنِ كَانَ ضَعِيفًا ٧٦

Alladhīna āmanū yuqātilūna fī sabīlillāhi walladhīna kafarū yuqātilūna fī sabīlit-tāghūti faqātilū awliyā'ash-shaytāni inna kaydash-shaytāni kāna da'īfā

Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu. 76

Maelezo ya chini

76 Walio isadiki Haki na wakaifuata, hupigana kwa ajili ya kulitukuza Neno la Mwenyezi Mungu, na uadilifu, na Haki. Na wale wanao pinga wakafanya inadi hupigana kwa ajili ya dhulma na uharibifu. Kwa hivyo hawa wamekuwa ni vipenzi vya Shetani. Basi enyi Waumini! Wapigeni vita hao, kwani wao ni wenzake Shetani na wasaidizi wake. Na jueni kuwa nyinyi mtawashinda tu kwa kuungwa mkono na Mwenyezi Mungu, kwani mpango wa Shetani, na ingawa mkubwa vipi ufisadi wake, ni dhaifu, hauna nguvu. Na Haki ndiyo yenye ushindi.