Surat An-Nisa, aya 75

4:75

وَمَا لَكُمۡ لَا تُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخۡرِجۡنَا مِنۡ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهۡلُهَا وَٱجۡعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّٗا وَٱجۡعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا ٧٥

Wamā lakum lā tuqātilūna fī sabīlillāhi wal-mustad'afīna minar-rijāli wan-nisā'i wal-wildānil-ladhīna yaqūlūna rabbanā akhrijnā min hādhihil-qaryatiz-zālimi ahluhā waj'al lanā mil ladunka waliyyan waj'al lanā mil ladunka nasīrā

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako. 75

Maelezo ya chini

75 Vipi inakufalieni kuwa msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na hali wanyonge, wanaume na wanawake na watoto wao, wanayayatika kuomba msaada wa kuwanusuru, huku wakimwomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu wakisema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutoe kwenye utawala wa hawa madhaalimu, na kwa nguvu zako na rehema yako tuwezeshe tuwe chini ya utawala wa Waumini; na tujaalie kutoka kwako mgombozi wa kutunusuru!