لَّٰكِنِ ٱللَّهُ يَشۡهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيۡكَۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلۡمِهِۦۖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَشۡهَدُونَۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا ١٦٦
Llākinillāhu yashhadu bimā anzala ilayka anzalahū bi'ilmihī wal-malā'ikatu yashhadūna wakafā billāhi shahīdā
Lakini Mwenyezi Mungu anayashuhudia aliyo kuteremshia wewe. Ameyateremsha kwa kujua kwake - na Malaika pia wanashuhudia. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. 166
Maelezo ya chini
166 Lakini ikiwa hao watu hawashuhudii kukusadikisha, basi Mwenyezi Mungu Mwenyewe anashuhudia kuwa aliyo kuteremshia ni sahihi. Hakika Yeye amekuteremshia hayo kwa hikima, na kwa mujibu wa ujuzi wake. Na Malaika nao wanashuhudia hayo kadhaalika. Na ewe Mtume! Yakutosha wewe ushahidi wa Mwenyezi Mungu, kuliko ushahidi wowote mwenginewe.