Surat An-Nisa, aya 100

4:100

۞ وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ١٠٠

Waman yuhājir fī sabīlillāhi yajid fil-ardi murāghaman kathīran wasa'atan waman yakhruj mim baytihī muhājiran ilallāhi warasūlihī thumma yudrikhul-mawtu faqad waqa'a ajruhū 'alallāhi wakānallāhu ghafūrar rahīmā

Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. 100

Maelezo ya chini

100 Anaye hama kutafuta njia za kuiwania Haki na kuiunga mkono, atakuta duniani kwingi endako ambako maadui wa Haki wanahizika. Na atapata wasaa wa uhuru, na makao ya hishima,na thawabu, na ujira mkubwa. Aliye toka kwake kuhamia dola ya hishima, ambayo ndiyo dola ya Mwenyezi Mungu na Mtumewe, kisha yakamdiriki mauti kabla hajafika endako, basi ujira wake umethibiti. Mwenyezi Mungu amemkirimu kwa kujiwajibishia kumlipa ujira wake, na kumghufiria na kumrehemu. Ni shani yake kughufiria na kurehemu.