وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا ١٠١
Wa idhā darabtum fil-ardi falaysa 'alaykum junāhun an taqsurū minas-salawāti in khiftum an yaftinakumul-ladhīna kafarū innal-kāfirīna kānū lakum 'aduwwam mubīnā
Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi. 101
Maelezo ya chini
101 Swala ni faridha isiyo epukika. Haiachiki Swala kwa ajili ya safari, lakini hana dhambi anaye fupisha Swala safarini. Watokao kwenda safari wakikhofia kuwa makafiri watawaletea ya kuwaudhi, wanaweza kufupisha Swala. Swala za rakaa nne zisaliwe rakaa mbili. Kutahadhari na kuingiliwa na makafiri ni waajibu, kwani wao ni maadui, na uadui wao uwazi.