Surat Al-Ma'idah, aya 27

5:27

۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱبۡنَيۡ ءَادَمَ بِٱلۡحَقِّ إِذۡ قَرَّبَا قُرۡبَانٗا فَتُقُبِّلَ مِنۡ أَحَدِهِمَا وَلَمۡ يُتَقَبَّلۡ مِنَ ٱلۡأٓخَرِ قَالَ لَأَقۡتُلَنَّكَۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ ٢٧

Watlu 'alayhim naba'abnay ādama bil-haqqi idh qarrabā qurbānan fatuqubbila min ahadihimā walam yutaqabbal minal-ākhari qāla la aqtulannaka qāla innamā yataqabbalullāhu minal-muttaqīn

Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu. 27

Maelezo ya chini

27 Hakika kupenda kutenda uadui ni tabia ya baadhi ya watu. Basi ewe Nabii! Wasomee Mayahudi - na wewe ni msema kweli - khabari za Haabila na Qaabila, wana wawili wa Adam. Kila mmoja alichinja dhabihu kama ni mhanga kwa kutaka kuruba kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alimkubalia mmoja kwa ajili ya usafi wa niya yake, na akamkatalia wa pili kwa kuwa niya yake haikuwa safi. Basi yule aliye kataliwa akamhusudu mwenzie na akamuahidi kuwa atamuuwa. Yule nduguye akamrudi kwa kumbainishia kuwa Mwenyezi Mungu hapokei a'mali ila kwa wachamngu walio safisha niya zao katika kule kutafuta kuruba.