Surat Al-Ma'idah, aya 26

5:26

قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيۡهِمۡۛ أَرۡبَعِينَ سَنَةٗۛ يَتِيهُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ فَلَا تَأۡسَ عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ ٢٦

Qāla fa innahā muharramatun 'alayhim arba'īna sanatan yatīhūna fil-ardi falā ta'sa 'alal-qawmil-fāsiqīn

(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi nchi hiyo wameharimishiwa muda wa miaka arubaini, watakuwa wakitanga-tanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wapotovu. 26

Maelezo ya chini

26 Mwenyezi Mungu akamuitikia Musa, akawapigia marfuku hao wakhalifu wasiingie nchi hiyo kwa muda wa miaka arubaini, wakipotea ovyo majangwani hawajui wendako wala watokako. Mwenyezi Mungu akamwambia Musa kama kumuasa: Usisikitike kwa masaibu yaliyo wasibu, kwani hawa ni wapotovu, wameiasi amri ya Mwenyezi Mungu.