Surat Al-Kahf, aya 24

18:24

إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ وَٱذۡكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَهۡدِيَنِ رَبِّي لِأَقۡرَبَ مِنۡ هَٰذَا رَشَدٗا ٢٤

Illā an yashā'allāhu wadhkur rabbaka idhā nasīta waqul 'asā an yahdiyani rabbī li aqraba min hādhā rashadā

Isipo kuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unapo sahau, na sema: Asaa Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu. 24

Maelezo ya chini

24 Ila kusema huko kuambatane na kupenda kwa Mwenyezi Mungu kwa kusema: Inshallah, yaani Mwenyezi Mungu akipenda. Na ukisahau jambo, basi kimbilia kumtaja Mwenyezi Mungu; na useme unapo azimia kufanya jambo na kuliambatanisha na kupenda kwa Mwenyezi Mungu: Huenda Mola wangu Mlezi akaniwafikisha kwenye bora kuliko nililo azimia kufanya, na lenye kuongoka zaidi.