Surat Al-Kahf, aya 25

18:25

وَلَبِثُواْ فِي كَهۡفِهِمۡ ثَلَٰثَ مِاْئَةٖ سِنِينَ وَٱزۡدَادُواْ تِسۡعٗا ٢٥

Walabithū fī kahfihim thalātha mi'atin sinīna wazdādū tis'ā

Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na wakazidisha tisa. 25

Maelezo ya chini

25 Na hakika hao vijana walikaa katika pango lao nao wamelala kwa miaka mia tatu, na ikazidi tisa. Aya hii inaonyesha ukweli wa ilimu ya Falaki (Astronomy), nayo ni kuwa ni miaka 300 kwa mwendo wa jua, na miaka 309 kwa hisabu ya mwezi unao fuatwa na Waislamu. Aya hii imeitangulia ilimu ya Falaki.