وَلِلۡمُطَلَّقَٰتِ مَتَٰعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ ٢٤١
Walil-mutallaqāti matā'u bil-ma'rūfi haqqan 'alal-muttaqīn
Na wanawake walio achwa wapewe cha kuwaliwaza kwa mujibu wa Sharia. Haya ni waajibu kwa wachamngu. 241
Maelezo ya chini
241 Na wanawake walio pewa T'alaka baada ya kuingia harusi wana haki wapewe mali ya kuwaliwaza. Wapewe kwa wema, kwa kadiri ya utajiri na umasikini wa mume. Kumcha Mwenyezi Mungu kunawajibisha hayo, na pia watu wa Imani wanalazimika na hayo.