وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا وَصِيَّةٗ لِّأَزۡوَٰجِهِم مَّتَٰعًا إِلَى ٱلۡحَوۡلِ غَيۡرَ إِخۡرَاجٖۚ فَإِنۡ خَرَجۡنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِي مَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعۡرُوفٖۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ٢٤٠
Walladhīna yutawaffawna minkum wayadharūna azwājan wasiyyatal li azwājihim matā'an ilal-hawli ghayra ikhrājin fa in kharajna falā junāha 'alaykum fī mā fa'alna fī anfusihinna mim ma'rūfin wallāhu 'azīzun hakīm
Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyo jifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 240
Maelezo ya chini
240 Wanao kufa miongoni mwenu wakaacha wake zao, Mwenyezi Mungu ameusia hao wanawake wafiwa wabaki nyumbani mwa waume zao muda wa mwaka mzima kwa maliwaza na kuwaondolea ukiwa. Wala hana haki yeyote kuwatoa. Wakitoka kwa khiari yao kabla ya mwaka kwisha basi hamna dhambi nyinyi wenye madaraka mkiwaachilia wajitendee wenyewe wapendalo kwa lisio vunja Sharia tukufu. Na mt'iini Mwenyezi Mungu katika hukumu zake, na tendeni Sharia alizo kutungieni kwani Yeye ni Muweza wa kumuadhibu anaye kwenda kinyume na amri yake, na Yeye ni Mwenye hikima iliyo pita ukomo. Hakuamrishini ila lenye maslaha yenu ijapo kuwa hikima yake imepindukia ujuzi wenu.