Surat Al-Baqarah, aya 242

2:242

كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ ٢٤٢

Kadhālika yubayyinullāhu lakum āyātihī la'allakum ta'qilūn

Namna hivi anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu. 242

Maelezo ya chini

242 Mwenyezi Mungu anakubainishieni hukumu zake, na neema zake, na Aya zake, kwa mfano wa bayana hizi na Sharia hizi zilizo wazi zenye kuleta maslaha, ili mpate kuzingatia na mpate kutenda yaliyo kheri.