Somo la 1 kati ya 3
Nitatawadhaje?
Kutoka Kurani
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا قُمۡتُمۡ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ فَٱغۡسِلُواْ وُجُوهَكُمۡ وَأَيۡدِيَكُمۡ إِلَى ٱلۡمَرَافِقِ وَٱمۡسَحُواْ بِرُءُوسِكُمۡ وَأَرۡجُلَكُمۡ إِلَى ٱلۡكَعۡبَيۡنِۚ وَإِن كُنتُمۡ جُنُبٗا فَٱطَّهَّرُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُم مِّنۡهُۚ مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجۡعَلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ حَرَجٖ وَلَٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمۡ وَلِيُتِمَّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴿٦﴾
Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.
Kutoka Sunna
Imepokelewa kutoka kwa Humran kijana wa Othman bin Affan alimuona Othman bin Affan akiomba kuletewa chombo cha udhu, akamimina juu ya mikono yake kutoka katika chombo chake, akaiosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wake wa kulia katika chombo, kisha akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga(akayatoa), kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara tatu, kisha akafuta kichwa chake, kisha akaosha kila mguu mara tatu, kisha akasema: Nilimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu wangu huu, na akasema: "Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia".
Maelezo
Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- alifundisha sifa ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa njia ya vitendo; Ili ueleweka vizuri zaidi, akaomba maji katika chombo, akamimina katika mikono yake mara tatu, na baada ya hapo aliingiza mkono wake wa kulia katika chombo, na akachukua maji akayazungusha kinywani mwake na akayatoa, kisha akavuta kwa pumzi yake kuja ndani ya pua yake, kisha akayatoa na akayapenga, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake pamoja na viwiko viwili mara tatu, kisha akapitisha mkono wake juu ya kichwa chake ukiwa umeloa kwa maji mara moja, kisha akaosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu.
Alipomaliza radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu huu, na akawapa bishara -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetawadha mfano wa udhu wake, na akaswali rakaa mbili, kwa utulivu na kuhudhuriasha moyo mbele ya Mola wake Mtukufu ndani yake, basi Allah atamlipa kwa udhu huu mkamilifu na kwa swala hii iliyotakaswa kwa kumsamehe yaliyotangulia katika madhambi yake.