إِنَّ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ ١٩٠
Inna fī khalqis-samāwāti wal-ardi wakhtilāfil-layli wan-nahāri la'āyātil li ulil-albāb
Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. 190
Maelezo ya chini
190 Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na viliomo ndani yao kwa vile vilivyo umbwa tangu mwanzo na mipango yake, na kukhitalifiana usiku na mchana kwa mwangaza na giza, kwa urefu wake na ufupi, zipo dalili na ishara zilizo wazi kwa watu wenye akili na kutambua za kuthibitisha Umoja wa Mwenyezi Mungu na Uwezo wake. "Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana ziko ishara kwa wenye akili" - Aya hii ina ukweli unao onyeshea taadhima ya Muumba. Mbingu ni moja katika Ishara za Mwenyezi Mungu inayo tubainikia kwetu kwa miale ya jua inayo piga juu ya anga linalo izunguka dunia. Miale hii inapo angukia chembe chembe na vumbi vumbi jembamba liliopo angani humulika mianga hiyo na kutawanyika kila upande. Huu mwanga mweupe kwa hakika ni mkusanyiko wa rangi zote zionekanazo. Hizi chembe chembe za angani huzimeza baadhi ya hizo rangi. Imedhihiri kuwa rangi yenye kuenea zaidi ni rangi ya kibuluu. Na hii inazidi kuzagaa linapo kuwa jua liko utosini, na ubuluu wake unapungua kidogo kidogo mpaka jua linapo kuwa upeo wa macho wakati wa magharibi au alfajiri. Wakati huo ile miale ya jua inakwenda masafa makubwa zaidi kabisa. Kwa hivyo zile chembe chembe za angani huzimeza rangi zote isipo kuwa rangi nyekundu. Usafi wa maneno ni: mwangaza wa mchana unahitaji miale ya jua na kuwepo vumbi la kutosha katika anga. Dalili ya hayo ni yale yaliyo tokea mwaka 1944 mbingu ilipo ingia kiza ghafla kati ya mchana. Jinsi ya kiza mchana ukawa kama usiku. Kwa wakati mfupi yakawa hayo, kisha mbingu ikawa nyekundu, kisha kidogo kidogo ikawa rangi ya machungwa, na kisha ya manjano mpaka mbingu ikarejea rangi yake ya tabia, baada ya saa au zaidi. Baadae ilibainika kuwa mambo hayo yalitokana na mripuko mbinguni likatokea jivu, likachukuliwa na upepo mbali mpaka Afrika ya kati na kaskazini, na kufika magharibi ya Asia. Huko ndiko ikaonekana hali hiyo katika pande za Syria. Maelezo yake ni kuwa vumbi lilioko hewani liliifunika nuru ya jua. Lilipo pungua jivu ulidhihiri mwangaza mwekundu na baadae wa manjano n.k. Mwanaadamu akipaa angani katika chombo atapitia matabaka yanayo khitalifiana sifa. Ataiona mbingu inazidi ubuluu mpaka akifika kwenye anga la nje lisio kuwa na hayo mavumbi n.k. ataona mbingu yote ni kiza kitupu kama kwamba ni usiku juu ya kuwa jua lipo juu. Kwa ufupi ni kuwa zipo mbingu nyingi si moja ziliyo pandana tabaka kwa tabaka kama maqubba, zinazo khitalifiana katika sifa zake na rangi zake. Haya ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliye takasika kuwa vyote viliomo mbinguni na ardhini vinamtukuza Yeye. Ama kukhitalifiana usiku na mchana, tumekwisha fahamu kuwa mwanga wa mchana unategemea miale ya jua kuanguka juu ya hili funiko la anga, lenye chembe chembe za vumbi kwa kiasi maalumu. Mwangaza huu ni mkali hata unaficha mwangaza unao toka kwenye nyota n.k. Ama wakati wa usiku mwangaza wa jua unapo fichika, inakuwa hapana katika anga isipo kuwa vumbi linalo tuzunguka na mianga dhaifu ya nyota. Kupishana usiku na mchana ni kwa sababu ya kuzunguka dunia kwa nafsi yake wenyewe, na tafauti ya misimu na kurefuka na kufupika usiku na mchana ni kwa mzunguko wa hii dunia kulizunguka jua. Na katika hikima yake Mwenyezi Mungu na uwezo wake ni kuwa kubadilika usiku na mchana, na kubadilika misimu ya joto na baridi, ni kutengeneza hali ya hewa iwe wastani, yaani kati na kati, kwa kusilihi maisha ya vilivyo hai.
ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَٰذَا بَٰطِلٗا سُبۡحَٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ ١٩١
Alladhīna yadhkurūnallāha qiyāman waqu'ūdan wa'alā junūbihim wayatafakkarūna fī khalqis-samāwāti wal-ardi rabbanā mā khalaqta hādhā bātilan subhānaka faqinā 'adhāban-nār
Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa Mbingu na Ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. 191
Maelezo ya chini
191 Ni shani ya wenye akili kuwa kila pahali wao wanahudhurisha katika nafsi zao adhama na utukufu wa Mwenyezi Mungu, wakiwa wamesimama au wamekaa au wamejinyoosha kitandani, na wanazingatia uumbaji wa mbingu na ardhi pamoja na viliomo ndani yake, na huku wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuumba haya ila kwa hikima uliyo ikadiria. Na Wewe umetakasika na kila upungufu. Bali umeumba hivi vyote kuwa ni dalili ya kudra yako, na ishara ya upeo wa hikima yako. Utuhifadhi na adhabu ya Moto kwa kutuwezesha kukut'ii.
رَبَّنَآ إِنَّكَ مَن تُدۡخِلِ ٱلنَّارَ فَقَدۡ أَخۡزَيۡتَهُۥۖ وَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ ١٩٢
Rabbanā innaka man tudkhilin-nāra faqad akhzaytahū wamā liz-zālimīna min ansār
Mola wetu Mlezi! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na walio dhulumu hawana wasaidizi. 192
Maelezo ya chini
192 Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Hakika mwenye kustahiki Moto na ukamuingiza, basi umempa hizaya. Na mwenye kudhulumu akastahiki Moto hana wa kumnusuru nao.
رَّبَّنَآ إِنَّنَا سَمِعۡنَا مُنَادِيٗا يُنَادِي لِلۡإِيمَٰنِ أَنۡ ءَامِنُواْ بِرَبِّكُمۡ فَـَٔامَنَّاۚ رَبَّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرۡ عَنَّا سَيِّـَٔاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ ٱلۡأَبۡرَارِ ١٩٣
Rrabbanā innanā sami'nā munādiyan yunādī lil-īmāni an āminū birabbikum fa'āmannā rabbanā faghfir lanā dhunūbanā wakaffir 'annā sayyi'ātinā watawaffanā ma'al-abrār
Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema. 193
Maelezo ya chini
193 Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Hakika sisi tumemsikia Mtume wako akiita watu wakuamini Wewe, nasi tukamt'ii na tukamuamini. Ewe Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu makubwa, na tufutie maovu yetu madogo madogo, na baada ya kufa kwetu tujaalie tuwe pamoja na waja wako walio bora.
رَبَّنَا وَءَاتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخۡزِنَا يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ إِنَّكَ لَا تُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ ١٩٤
Rabbanā wa ātinā mā wa'attanā 'alā rusulika walā tukhzinā yawmal-qiyāmati innaka lā tukhliful-mī'ād
Mola wetu Mlezi! Na utupe uliyo tuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji miadi. 194
Maelezo ya chini
194 Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Tupe uliyo tuahidi kwa ndimi za Mitume yako, nayo ni ushindi na kuungwa mkono duniani. Wala usituingize Motoni ukatuhizi Siku ya Kiyama. Shani yako ni kuwa huendi kinyume na miadi yako.
فَٱسۡتَجَابَ لَهُمۡ رَبُّهُمۡ أَنِّي لَآ أُضِيعُ عَمَلَ عَٰمِلٖ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰۖ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۖ فَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ وَأُخۡرِجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَأُوذُواْ فِي سَبِيلِي وَقَٰتَلُواْ وَقُتِلُواْ لَأُكَفِّرَنَّ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَلَأُدۡخِلَنَّهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ ثَوَابٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلثَّوَابِ ١٩٥
Fastajāba lahum rabbuhum annī lā udī'u 'amala 'āmilim minkum min dhakarin aw unthā ba'dukum mim ba'din falladhīna hājarū wa ukhrijū min diyārihim wa ūdhū fī sabīlī waqātalū waqutilū la ukaffiranna 'anhum sayyi'ātihim wala'udkhilannahum jannātin tajrī min tahtihal-anhāru thawābam min 'indillāhi wallāhu 'indahū husnuth-thawāb
Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi. Basi walio hama, na walio tolewa makwao, na wakateswa katika Njia yangu, na wakapigana, na wakauliwa, kwa yakini Mimi nitawafutia makosa yao, na kwa yakini nitawaingiza katika Mabustani yanayo pita mito kati yake. Hayo ndiyo malipo yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu kwake yapo malipo mema kabisa. 195
Maelezo ya chini
195 Mola wao Mlezi aliwaitikia dua yao, akiwabainishia kuwa Yeye hampotezei mtendaji thawabu za vitendo vyake, sawa sawa akiwa mwanamume au mwanamke, kwani mwanamke anatokana na mwanamume, na mwanamume anatokana na mwanamke. Basi wale walio hajiri, wakahama, wakagura, wanatafuta radhi ya Mwenyezi Mungu, na wakatolewa makwao, na wakapata mateso katika Sabili Llahi, Njia ya Mwenyezi Mungu, wakapigana vita, na wakakhatirisha kuuwawa, bali wakauliwa walio uliwa, Mwenyezi Mungu amejilazimisha Mwenyewe kuwasamehe madhambi yao, na kuwatia kwenye Mabustani yenye kupita kati yake mito, kuwa ni malipo matukufu yaliyo bora kutokana na Mwenyezi Mungu. Na kwa Mwenyezi Mungu peke yake, ndio yako malipo mazuri.
لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ ١٩٦
Lā yaghurrannaka taqallubul-ladhīna kafarū fil-bilād
Kabisa kusikudanganye kubakia kutangatanga kwa walio kufuru katika nchi. 196
Maelezo ya chini
196 Usiathirike, ewe Nabii, kwa kuwaona makafiri wamo katika starehe za neema, na biashara na uchumi unawaendea, wakienda huku na huku katika nchi.
مَتَٰعٞ قَلِيلٞ ثُمَّ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ ١٩٧
Matā'un qalīlun thumma ma'wāhum jahannamu wabi'sal-mihād
Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makaazi yao yatakuwa Jahannamu. Na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia. 197
Maelezo ya chini
197 Hizo ni starehe za kupita njia, na kila kipitacho ni duni. Kisha marejeo ya daima watayo ishia ni Jahannamu. Na hapana makaazi maovu kama Jahannamu.
لَٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ رَبَّهُمۡ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا نُزُلٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۗ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّلۡأَبۡرَارِ ١٩٨
Lākinil-ladhīnat-taqaw rabbahum lahum jannātun tajrī min tahtihal-anhāru khālidīna fīhā nuzulam min 'indillāhi wamā 'indallāhi khayrul lil-abrār
Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata Mabustani yanayo pita mito kati yake. Watadumu humo. Hayo ni makaribisho yao yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na vilioko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa watu wema. 198
Maelezo ya chini
198 Hayo ndiyo malipo ya makafiri. Ama walio muamini Mwenyezi Mungu wakamwogopa Mola wao Mlezi watapata Mabustani yapitayo mito kati yake, watadumu humo daima, kuwa ni wageni walio pokewa kwa ukarimu na Mwenyezi Mungu, Subhanahu, Aliye takasika. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio mazuri kwa watu wema kuliko hayo wanayo starehea makafiri ambayo yataondoka, hayadumu.
وَإِنَّ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَمَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِمۡ خَٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشۡتَرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ ١٩٩
Wa inna min ahlil-kitābi laman yu'minu billāhi wamā unzila ilaykum wamā unzila ilayhim khāshi'īna lillāhi lā yashtarūna bi'āyātillāhi thamanan qalīlan ulā'ika lahum ajruhum 'inda rabbihim innallāha sarī'ul-hisāb
Hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na yaliyo teremshwa kwenu na yaliyo teremshwa kwao, wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawabadili Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani duni. Hao wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. 199
Maelezo ya chini
199 Hakika baadhi ya Watu wa Kitabu, Mayahudi na Wakristo, wanamuamini Mwenyezi Mungu, na wanaamini aliyo teremshiwa Nabii Muhammad s.a.w. na walio teremshiwa Mitume walio kuwa kabla yake. Utawaona wanamnyenyekea Mwenyezi Mungu, na wanakuwa wanyonge kwake, wala hawabadilishi bayana zilizo dhaahiri kwa ajili ya kutafuta pato la duniani. Hilo nalingawa kubwa ni kitu duni. Hawa wana malipo ya ukamilifu kwa Mola wao Mlezi katika makaazi ya kuridhisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu, hashindwi kuzidhibiti 'amali zao zote na kuwahisabia. Yeye ni Muweza wa hayo na malipo yake yatawafika bila ya shaka.
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱصۡبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ٢٠٠
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanusbirū wasābirū warābitū wattaqullāha la'allakum tuflihūn
Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa. 200
Maelezo ya chini
200 Enyi mlio amini! Shikamaneni na subira, na mwashinde maadui zenu katika kusubiri. Na kaeni macho kuilinda mipaka, na mkhofini Mola Mlezi wenu. Katika haya yote ndio mtaraji kufanikiwa. (Jee! Baada ya kuijua Qur'ani yamfalia Muislamu kusema kuwa dini ni kitu mbali na siyasa? Vipi uamrishe mema, ukataze maovu, uhukumu, ukatibiane mikataba na dola nyengine, ukusanye zaka na kuzigawa, upigane Jihadi, ulinde mipaka n.k., n.k. na uiepuke siyasa? Amesema Prof. Khurshid Ahmad: "Uislamu si dini kwa maana ya ovyo ovyo kama lilivyo potoshwa neno hilo, yaani kuwa umemkhusu mtu maisha yake ya binafsi tu. Ni mwendo kaamili wa maisha, unao angalia kila midani ya uhai wa binaadamu. Uislamu ni uwongozi katika kila nyendo za maisha - za binafsi na za jamii, za kimwili na kiroho, za uchumi na siyasa, za sharia na mila, za taifa na za mataifa."--Uislamu, Maana na Ujumbe wake uk. 37)
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.