Surat Hud, aya 69

11:69

وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ ٦٩

Walaqad jā'at rusulunā ibrāhīma bil-bushrā qālū salāman qāla salāmun famā labitha an jā'a bi'ijlin hanīdh

Na wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: Salama! Hakukaa ila mara akaleta ndama wa kuchoma. 69

Maelezo ya chini

69 Na Sisi tuliwatuma Malaika kwa Ibrahim wampe bishara njema yeye na mkewe kuwa watapata mwana. Waliwasalimu kwa kauli ya: Salama! Naye akarejesha amkio lao kwa kusema: Salama! Upesi upesi akenda kuwatengezea ndama aliye nona wa kuchoma ili wale.