كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَاْ كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّثَمُودَ ٦٨
Ka al lam yaghnaw fīhā alā inna thamūda kafarū rabbahum alā bu'dal lithamūd
Kama kwamba hawakuwako huko. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud wamepotelea mbali! 68
Maelezo ya chini
68 Mambo yao yakawaishia, na alama zao zikaondoka katika majumba yao. Wakawa kama kwamba hawajapata kuwamo humo. Hali yao ni ya kumzindua kila mwenye akili azingatie, na ajue kuwa hao kaumu ya Thamud walizikanya Ishara za aliye waumba!! Na kwa sababu ya hayo ndio wakaangamizwa na wakatengwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu.